Advertisements

Tuesday, April 22, 2014

NANDO KUTOA KITABU KITAKACHO CHAMBUA MAISHA

Baada ya kua kimya kwa mda mrefu, aliyekua mwakilishi wa Tanzania katika Jumba la Big Brother Afrika mwaka jana amerudi Tanzania akitokea Marekani alipokua akikaa. Taarifa tulizozipata kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers zinasema kuwa Nando amerudi Tanzania lengo kubwa likiwa ni kuandika kitabu kitachoelezea Maisha yake aliyopitia hadi alipo sasa.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Nyemo aliandika haya kuhusiana na kitabu hicho
Huyu ni Nando, Mwakilishi wa Tanzania katika Jumba la Big Brother mwaka jana ambapo licha ya kutokutoka kifua mbele kama mshindi lakini ukitamka jina la NANDO afrika inatambua vyema ni nani na kwa kiasi kikubwa aliweza kuiwakilisha vyema Tanzania. Baada ya kutoka nchini Marekani, sasa yupo nchini Tanzania kwa kazi moja tu ya kuandika kitabu cha maisha yake, kitabu kilichojaa historia yenye kusisimua iliyompelekea kukataliwa na baadhi ya ndugu, kunusurika kufa, kutengwa, kunyanyaswa na kufanyiwa mambo mengine ambayo kama yangemkuta mtu mwenye moyo mwepesi, sasa hivi tungemuita marehemu.

Pamoja na maneno mengi, shukrani kwa Mkurugenzi wangu, Eric Shigongo kwa kunipa ruhusa ya kukiandika kitabu cha Mtanzania huyu, mwakilishi wa Tanzania katika Jumba la Big Brother.

Uandishi umeanza, kwenye kila mstari ninaoandika, ninaguna na kumuuliza ‘Ulikuwa ukisubiri nini? Mbona ni mateso makubwa hivi! Kweli umestahili kuwa hapo ulipo’
Kitabu hiki kikikamilika, kitauzwa Afrika nzima na kitaandikwa kwa lugha mbili, Kingereza na Kiswahili. Baada ya kuuzwa Afrika, pia kitapelekwa mpaka nchini Marekani anapoishi kwa sasa. Wewe kama Mtanzania unayepitia mambo mbalimbali hautakiwi kukikosa, ni kitabu kilichojaa msisimko mkubwa.

Pamoja na kitabu hicho, pia utapewa CD yake ya Video inayohusu makala ya maisha yake. Kaa mkao wa kula. Hautakiwi kukikosa hiki kitabu. Bei haijajulikana”.
Credit:Gongamix

2 comments:

Anonymous said...

Nami naandika kitabu sababu nimefaanikiwa sana. Nataka watu wajifunze kutokana na mafanikio yangu.

Anonymous said...

Hahahahaha we mkali