Marehemu Muhidini Gurumo atakumbukwa sana na wasanii wote Tanzania Alikuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wote alikuwa yuko mstari wa mbele kuwatetea wasanii na maslahi yao alikuwa anahimiza wasanii kujitambua kutokuogopa na kusimamia haki yako nakumbuka kuna wakati tukiwa kwenye semina ya wasanii Bagamoyo kuna mtu alisimama anataka kuelezea maswala ya wasanii alimuliza naomba utueleze unatoka kikundi au bendi gani au unapiga chombo gani aliposita alimwambia tunaomba kaka ukae chini Aliamini msanii ndiye anayeweza kuelezea maswala yanayomkabili sio mwingine kwa ujasiri huu na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwenye sanaa ya muziki aliweza kuchaguliwa kiongozi kila Bendi aliyoenda zikiwemo Juwata, DDC Mlimani Park na Safari sound.
Licha ya kuwa kiongozi alikuwa mtunzi muimbaji na mbunifu wa mitindo kama Msondo ngoma Sikinde ngoma ya ukae na ndekule, mzee Muhidini niliwahi kufanya nae kazi kwa karibu sana wakati nikiwa kiongozi wa D D C KIBISA NGOMA naye Akiwa D D C MLIMANI PARK kwenye miaka ya 80 tumekuwa tukikutana kwenye shughuli mbalimbali zinazohusu sanaa.
Ninatoa pole sana kwa bendi aliyoipigia mara ya mwisho MSONDO NGOMA mke wake watoto wasanii wote Tanzania na wapenzi wote wa muziki Tanzania.
Ameacha pengo si kwa familia yake bali kwa waTanzania wote wapenzi wa muziki ameondoka wakati bado ushauri tulikuwa tunauhitaji tunamuomba mwenyeenzi MUNGU aiweke rohoyake mahalapema peponi AMINA MIMI SALIMA MOSHI msanii mwenzake
No comments:
Post a Comment