Advertisements

Thursday, April 17, 2014

Shamim Khan adai maoni Bakwata yamechakachuliwa

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Shamim Khan, amedai kuwa maoni yaliyotolewa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) yamechakachuliwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni ya wananchi.

Amesema maoni ya Bakwata yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba si yale yaliyotolewa na baraza hilo kwani halijapendekeza muundo wowote wa Muungano, lakini kwenye rasimu imelezwa kuwa limependekeza muundo wa serikali tatu.

Alitoa madai hayo bungeni, wakati akichangia mjadala wa sura ya kwanza inayohusu Jina la Jamhuri na ya sita inayohusu muundo wa Muungano.

“Mimi ni mjumbe wa Baraza la Bakwata lililotoa maoni, nimeshangazwa sana na jambo hilo, ili kujiridhisha nimewasiliana na Katibu Mkuu wa Bakwata na Mufti Issa Shaban Simba, wote wamekanusha baraza kutoa maoni hayo,” alisema.

Shamim alisema walitoa maoni ya kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi itakayohudumiwa na Serikali na kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC), lakini maoni hayo hayakuwekwa kwenye rasimu.

1 comment:

Anonymous said...

na bado uko ccm au? si unaona kasheshe hiii