ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 25, 2014

SHEREHE ZA UZINDUZI WA SHINA LA (CCM) MARYLAND

Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na Balozi Bi.Libereta Mulamula wakwanza Kulia na Ndugu Mrisho Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Shina la CCM hapa MaryLand-Marekani hii leo alipowasili Washington Airport.
Uongozi wa shina la (CCM) Maryland unawaalika wanachama wa ccm, wapenzi wa ccm na watanzania wote kwa ujumla kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa shina la (CCM) Maryland. Sherehe zitafanyika Tarehe 27 mwezi huu wa nne, 2014 katika ukumbi wa Tabeer Restaurant kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku. Kutakua na chakula, vinywaji pamoja na viburudisho vya aina mbalimbali.
Pia kwa wale watakaopenda kujiunga na shina hili, form za uanachama zitatolewa siku hiyo.
Binadamu Wote ni sawa!! Karibuni waTanzania Wote tusherehekee!!
Tangazo Limetolewa na UONGOZI wa Shina (CCM) Maryland.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

2 comments:

Anonymous said...

Haya mashina ya ccm huku ya kazi gani, wakati watu wanakufa kwa njaa huko nyumbani, hizo fedha kama mnataka si mzitume huko nyumbani zisaidie mahospitali na shule..!?

Anonymous said...

Hongereni