ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 28, 2014

TASWIRA UZINDUZI WA SHINA LA CCM MALYLAND,MH:MWIGULU AVUNA WANACHAMA WAPYA

Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akiwasili Ukumbini hapa Maryland kufungua Shina la Chama cha Mapinduzi hii leo.
 
 Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia Jambo na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV wakati akiwasili kwenye Uzinduzi wa Shina la CCM-Maryland.
Naibu katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiwapungia Mkono Wana-CCM waliofika kwenye Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland hapa Marekani.
 Comrade Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliofika kwenye tukio la Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland.
 
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na MC wa Shughuli ya Ufunguzi wa Shina la CCM akiwajibika kuweka ratiba sawa Ukumbini,
Makada watiifu wa Chama cha Mapinduzi hapa Maryland.
Watanzania na Wana-CCM wakiwa tayari Kuitumikia Nchi yao na Chama chao.
Wadau wakipata Ukodak.
 Mh:Mwigulu Nchemba akipokea kadi ya aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA ambaye ameamua Kuachana na Chama hicho na Kujiunga na Chama cha Mapinduzi,
Loveness Mamuya kada Mtiifu wa CCM na Muasisi wa harakati za CCM hapa Marekani akiwasalimia wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliofika kwenye Uzinduzi wa Shina la CCM Maryland.
 Mwenyekiti wa CCM Kwa Watanzania waliopo DMV akizungumza na Wana-CCM Umuhimu wa Kujiunga na Chama cha Mapinduzi,Pia amezungumzia Maadili ya Watanzania wanaoishi nje ya Nchi hususani Marekani Kutukana Viongozi Mitandaoni"Huo sio Utamaduni Wetu Watanzania" alisema.
Wana-CCM Wakipata Ukodak.
Hapa ni Mwendo wa CCM nambari One.
 Makada Watiifu wa Chama cha Maopinduzi hapa Maryland.
Sehemu ya Wana-CCM waliofika kwenye Uzinduzi wa Shina la CCM Maryland wakisikiliza kwa makini Ujumbe kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Mh:Mwigulu NChemba.
 Makada wa Chama cha Mapinduzi wakipata Ukodak.Mama Nchemba (Mke wa Mh:Mwigulu) akisalimia Wana-CCM waliofika Kwenye
hafla ya Uzinguzi wa Shina la CCM Marly Land
Miss Temeke akiwa na Mmewake kwenye uzindui wa Tawi la CCM-Maryland.Mwanachama wa CCM akiuliza Swali kwa Mh:Kuhusu Urai Pacha na namna Chama cha mapinduzi kilivyolichukulia Swala hilo.Mh:Mwigulu Nchemba amesema Chama cha Mapinduzi kwenye rasimu mpya Kimependekeza Urai pacha na Kimejipanga Kuhakikisha jambo hilo linachukuliwa kwa Uzito wake na hatimaye Uraia pacha Upatikane.
 Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia jambo mara baada ya Mwanachama wa CCM kusema kutokana na Mwenendo wa Siasa zake atakuwa kuwa Kiongozi Mkubwa katika Nchi hii,na Wana-CCM wataendelea Kumuunga Mkono katika kazi zake.Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-DMV -CCM akitoa Ombi rasmi kuwa Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba awe mlezi wa Jumuia ya Wanawake=DMV.
 Mh:Mwigulu Nchemba akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye hafla ya Ufunguzi wa Shina la CCM-Marland-Marekani.
Mwenyekiti wa Shina la CCM-Maryland Ndugu Mrisho Mzese akishiriki Chakula kilichoandaliwa kwenye Ufunguzi huo wa shina.Furaha ya Kukutana na Kiongozi wa Kitaifa ni pamoja na Kuweka Kumbukumbu ya Picha kama hivi.Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake-CCM hapa Marekani(Watatu kutoka Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wanawake walifika kwenye hafla ya Uzinduzi wa Shina la CCM-Maryland.

Viongozi wa Chama wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu-CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba kupiga picha ya pamoja na Wanachama wapya wa Chama cha mapinduzi.Hii leo Mh:Mwigulu Nchemba amepokea Wanachama 8 wapya waliojinga na CCM.

Kutoka Washington-DC.
Naibu katibu Mkuu CCM-Bara  Mh:Mwigulu Nchemba hii leo tar 27/04/2014 amezindua Shina la Chama cha Mapinduzi hapa Maryland tayari kwa kuanza kuitumikia CCM na Wanachama wake.Ufunguzi wa Shina hili ni mwendelezo wa kuhakikisha Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanakuwa katika Mfumo mmoja wa Kichama.
Akizungumza na Watanzanai waliofika kwenye Uzinduzi huo,Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kwa Wana-CCM wanatakiwa kujenga mazingira ya Kuwa pamoja mara kwa Mara kwaajili ya Kujenga Umoja na Mshikamano hasa Ukizingatia wapo Mbali na Nyumbani Tanzania.
"Umoja wenu ndio Ngao yenu kwa hapa Marekani,Naomba sana Mshiriki kwenye Jumuia zenu na mshiriki kwenye Shughuli za pamoja zikiwamo hizi za Kisiasa,Haitakuwa afya Kufunga Mashina na Matawi ya CCM Kwaajili ya Kuvunja Umoja wetu,Tutumie Mashina haya Kutuimarisha zaidi"alisema Nchemba.
Mbali na hilo na Kudumisha Umoja,Mh:Nchemba ameendelea kusisitiza kuwa Mchakato wa Katiba Mpya ni jambo Zuri sana lakini Kukosekana kwa Utashi wa Kisiasa kwa Viongozi wa Kisiasa kunapeleka katiba ama kutopatikana au Kuchelewa kupatikana.Hivyo ameomba Watanzania waliopo Marekani na Nchi nyingine kaucha kushabikia Mambo yasiyokuwa na tija kwa Taifa lao ambayo yatapelekea Utengano.
Zaidi ameahidi Viongozi wa CCM Wataandaliwa Semina kwaajili kupata Mafunzo ya Kuwa Kiongozi Mwadilifu na Mzalendo kwa Chama na Taifa letu.
Picha/Maelezo na Sanga-Festo /Washington DC

No comments: