WANAFUNZI wa
Shule ya Msingi Liami wilayani Ifakara mkoani Morogoro (jina
limehifadhiwa), amebakwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Mei 5, mwaka
huu nyumbani kwa bibi yake.
Mwanafunzi ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa hoi hospitali baada ya kubakwa.
Akizungumza
mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Neema Ally akiwa wodi A ya
watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema mtoto wao alienda
nyumbani kwa bibi yake kulala baada ya kumaliza kula kwa wazazi wake.
Alisema
watu waliofanya unyama huo, pia waliiba baiskeli kabla ya mtoto wao
kuokolewa na wasamaria wema waliosikia mayowe yake ya kuomba msaada
ambapo walimkuta akitokwa na povu mdomoni.
Alisema wasamaria wema hao walimkuta mtoto wake akiwa amepoteza fahamu kutokana na kukabwa koo wakati akifanyiwa kitendo hicho.
“Hali
ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa Hospitali ya St. Frances, Ifakara
ambako nako hakukaa, akahamishiwa hapa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Mama wa mtoto huyo akiwa na binti yake hospitalini.
“Ilimchukua
muda wa siku tatu mtoto kupata fahamu, nawashukuru Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Ifakara kwa kutoa gari la kubebea wagonjwa kwa
haraka ili kunusuru maisha ya mwanangu na fedha,” alisema Neema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment