ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 5, 2014

FLAVIANA MATATA BLACK BEAUTY

African hairstyle imekuwa gumzo sasa hivi duniani kwenye upande wa jamii ya watu weusi. Kwanini “Weaving” na isiwe style ambayo tutajivunia na “Unique Black African Hair” ambazo tumepewa na mungu?.
Hata kama ni “Kipiri Piri” lakini zinapendeza katika kichwa na muonekano wa mwanamke wa kiafrika”
Mwanamitindo Flaviana Matata ni mmoja kati ya wanadada wa ambao tokea zamani yeye style yake ya nywele ni “Natural” . Mwanamitindo huyu tokea ameanza kazi hizo Na sasa kupata “Recognitions” katika fani ya “Mitindo” hapa nchini na nje ya nchi na mpaka kufikia hivi sasa yupo ndani ya TOP 20 ya Global African Models hatujawahi kuona “Human Hair, Weaving, Wigi, Brazilian” au chochote ambacho kiliondoa “root” ya muonekano wa Flaviana popote pale alipo. Flaviana Mara chache sana utamuona amevaa “Weaving Hair” pale tu kama yupo kwenye “photo-shoot” ambayo imemlazimu kuvaa lakini la hasha hata kwenye “Runway” utamuona mwanadada Flaviana akiwa kwenye nywele zake za asili.
Kwanini Style hii isiwe Style ya wanawake wa kimashariki mwa afrika (East Afrika) kutengeneza uniqueness ya kiafrika?
Style hii ya nywele imekua gumzo sana kimataifa kwa sasa duniani na wanawake wengi mashuhuri duniani wameonyesha mfano huo. Kwa East Africa tunae mwanadada “Lupita Nyong’o” kutoka nchini Kenya ambae baada ya kupata nafasi ya kushinda OSCARS Awards kutokana na filamu aliyoicheza ijulikanayo kama “12 Years Of Slave”, imesababisha gumzo hilo kuwa kubwa zaidi na kusababisha wanawake wengi kuacha uvaaji wa nywele bandia na kuamua kubaki na nywele zao za asili.
Kituo kimoja cha cha radio nchini England kijulikanacho kama “Capital 1XTRA” siku chache zilizopita kilikua na campaign kuzungumzia kwanini wanawake wa kiafrika wanavaa nywele kutengeneza muonekano wa watu weupe wenye nywele laini, wakati muonekano wetu wa asili ni bora na tunaonekana tofauti kiasi ambacho wao tunaowaiga hawawezi kufanya wakaonekana kama waafrika.
“Why African Women wear straight Hair and neglect the Beauty of Natural Hair that make a Uniqueness of being an African Woman?” – Kojo:
Creadit:Gongamix

1 comment:

Anonymous said...

That's is nice,but remember beauty is in the eye of the beholder.short hair,long hair,weave,clips it does not matter.thx