ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 28, 2014

Ibada Maalum ya Miaka Mitano ya Ibada ya Kiswahili na Kusimikwa Mchungaji Ipyana Mwakabonga - Juni 1, 2014 Kuanzia 3:30pm

 Anza Siku njema na NENO la MUNGU kila siku kwa kutembelea Ibada ya Kiswahili website na Ukurasa wa Ibada ya Kiswahili kwenye Facebook.
**   **   **            ** www.iykcolumbus.org **         **   **   ** 

NENO LA LEO: Marko 11:25-26, Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.

TAFAKARI: Mojawapo ya sababu inazuia kujibiwa maombi ni hali ya kutokusamehe. Wengi tunajiuliza kwa nini huwa hatujibiwi maombi kwa haraka na uhakika kama baadhi ya Wakristo. Jibu ni kwamba kama unaenda mbele za Mungu ukiwa umewashikilia watu moyoni mwako na kama unaishi maisha ya visasi basi uwe na hakika kuwa hiyo ndo sababu inayomzuia Mungu kukujibu maombi yako. Kama hutoweza kumsamehe jirani yako, na Mungu hatakusamehe wewe. Na kama hujasemehewa basi utakuwa bado na dhambi zako, na Mungu huwa ajibu maombi ya mwenye dhambi na ndo maana wengi wetu tumekwama katika hali tulizo nazo bila kujua tufanyeje.

SALA: Mungu wangu, leo hii ninawasemehe watu wote waliowahi kunikosea na kuniumiza. Nawachilia moyoni mwangu, naomba na wewe unisamehe na kunirehemu. Upate kusikiliza maombi yangu na kunijibu. Kwa Jina la Yesu, (c) IYK_NENO

No comments: