Hiyo ni zahanati ya serikali iliyoko Kunduchi Mtongani. Nilikwenda hapo mara ya kwanza kama miezi mitatu iliyopita; nilishangaa kuona wahudumu walio “serious”, maabara inayofanya kazi na vifaa vipo, pia na madawa yapo. Na kila dawa inayotoka inarekodiwa!
Nimerudi hapo juzi, nikashangaa kukuta ukarabati mkubwa uliofanywa, ndani ya
muda mfupi sana. Tiles nyeupe kote, mpaka majengo ya nyuma,
choo safi namaua yanayohudumiwa. Pia huduma za uhakika. Nilitaka
kupima malaria, nikakuta mtu wa maabara ameishaondoka, maana muda wake ulikuwa umekwisha; daktari wa kike, ambaye yuko pale siku zote, akaja mwenyewe kunitoa damu na kupima. Nilimshukuru sana, maana nageweza kuniambia njoo kesho, mwenyewe kaondoka.

Nilimuuliza daktari wanafanyaje kuitunza zahanati yao; akajibu kuwa, kukiwa na bodi ya uhakika, pesa za TASAF zikija zinafanya kazi. Akanionyesha jengo la jirani la mwaka 47 linalokaribia kuporomoka , pia la serikali akasema, “wale pia wanapata pesa kama sisi”!! Nikajua wale zao ni “tumbo street” tu!!
Nawapongeza sana uongozi wa zahanati hii, kwa kazi nzuri sana wanayofanya. Kumbe watu wakiamua, mambo ya serikali yanawezekana!!

LKK
Hongereni sana uongozi mzima wa zahanati hii.Ni mifano michache ya kuigwa TZ.
ReplyDeleteProbably the only successful project i have ever heard of, hela hazikuliwa na wajanja hapo. Hongera na Mola awajalie neema,
ReplyDelete