Advertisements

Saturday, May 10, 2014

KUTUNZA WAZEE NYUMBANI TANZANIA NI JUKUMU LA NANI, WAZEE WASIO KUWA NA WATOTO WATUNZWE NA NANI


Andrea ni mwanafunzi kutoka Swiss aliyeishi Tanzania akifuatilia matunzo ya Wazee wetu wa Kitanzania wanayoyapata wakiwa nyumbani, sasa hivi Andrea yupo Marekani na alijaribu kukutana na baadhi ya Watanzania na kuongelea swala la utunzaji wazee wetu ni jukumu la nani na kama juhudi za kutunza wazee hazitoshi ni nani walaumiwe kama ilivyojengwa vituo vya kulelea watoto walikosa wazazi wao  je kuna haja ya kujenga vituo vya kulelea wazee waliokosa watoto wao? hapo chini Andrea ameleta maswali tujaribu kuchangia kuhusu swala hili la Wazee


1)nani ana jukumu kwa kutunza wazee tanzania? na vipi? (ni familia? serekali? taasisi binafsi? ...) leo na baadaye/wakati ujao? so whos obligation is it actually to take care of wazee?


2)kuna mahitaji gani kwenye maisha ya wazee? na tunahitaji kufanya nini? (au serekali au nani inahitaji kufanya nini?) what needs to be done and by whom, as there will be more wazee in the future?


3)Wazantania ambao wanakaa nje ya tanzania wanaumuhimu gani au wanafikiria nini kuhusu wazee? that is their importance/responsibility when it comes to care of their elders?

all over the world people get older and older, also in Tanzania... na kuna watu ambao wanasema wazee kotoka Tanzania wanapata matunzo vizuri kwa sababu kuwa karibu na familia... lakini kuna wengine wanasema, Tanzania kuna shida kwa sababu wazee hawapati matibabu na masaada kutoka serakali, na watoto lwao wengine wakiwa hawana uwezo wa kifedha wa kuwatunza wazee wao.

This just came into my mind when thinking about what do discuss in your blog about wazee... maybe it is of use and maybe not...

your blog is so rich, napenda sana kuisoma!
ninakutakia jioni njema,
greetings kutoka Boston,
Andrea

3 comments:

Anonymous said...

nakubaliana kabisa na wewe bwana Andrea na mada uliyoitoa. Kweli hilo suala ni la muhimu sana, sidhani kama Seriakli yetu inalijua hilo. Lakini hatujachelewa, linaweza kuanza kufanyiwa kazi. Iweke mada hiyo mezani na ianze kufanyiwa kazi hadi Serikalini ili ipate bajeti. Hadi Bungeni itambuliwe maana hao wabunge wenyewe sijui kama wanafikiria hilo au wanafikiria watakuja zeeka. Kwanza Serikalini ipate bajeti.

Anonymous said...

nakubaliana kabisa na wewe bwana Andrea na mada uliyoitoa. Kweli hilo suala ni la muhimu sana, sidhani kama Seriakli yetu inalijua hilo. Lakini hatujachelewa, linaweza kuanza kufanyiwa kazi. Iweke mada hiyo mezani na ianze kufanyiwa kazi hadi Serikalini ili ipate bajeti. Hadi Bungeni itambuliwe maana hao wabunge wenyewe sijui kama wanafikiria hilo au wanafikiria watakuja zeeka. Kwanza Serikalini ipate bajeti.

Anonymous said...


1. kama hao wazee walikuwa na uwezo wa kufanya kazi wakiwa vijana waliweza kuchangia kwenye uchumi wa Taifa kwa kufanya kazi na kuweka michango yao kwenye taasisi za akiba. Itakuwa si busara kabisa serikali kutoa fedha ambazo collectively zingewasaidia watanzania wote ziwasaidie wachache.Fedha hizo badala ya kutumiwa vibaya zingeweza kuboresha huduma za afya kwa wazee wote bure.
2.0 Walemavu na walio na matatizo ya kiafya wasaidiwe bure.
Vinginevyo sikubaliani na kusaidia wazee wote kwa kuwapa fedha kila mwisho wa mwezi huu si utaratibu hata rais Kikwete alisema hizo fedha zitatoka wapi kwa kuwalipia wazee ambayo hawajachangia chochote katika mifuko ya akiba au hawakujiwekea akiba. Ikiwa ingawa naelewa haiwezekani kila mzee atapewa fedha kila mwisho wa mwezi itakuwa si kuwatendea haki wazee waliolipa au waliochangia fedha kwenye mfuko.

Tanzania haina uwezo wa kuwalipia wazee fedha za kuishi kila mwezi bure....haiwezekani, hata nchi tajiri hawawezi.