Mnamo tarehe 28 Aprili 2014 Mheshimiwa Mzee Kenneth David Kaunda (KK), Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Zambia alifikisha miaka tisini (90). Sherehe kubwa iliandaliwa siku hiyo ambapo Mama Maria Nyerere alialikwa lakini kwa sababu zisizozuilika hakuweza kuhudhuria. Ili kukamilisha nia hiyo Mama Nyerere akamtuma mwanae Mheshimiwa Makongoro Nyerere ambae pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kuja kuwasilisha salamu za pongezi zake binafsi na za familia ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Makongoro pamoja na salamu alimkabidhi Mheshimiwa Mzee Kaunda zawadi ya kinyago ambacho kilitafsiriwa kama Umoja na Mshikamano. Katika hafla hiyo aliongozana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mheshimiwa Grace Mujuma.
Baada ya kupokea salaam na kinyago Mzee Kaunda alitoa shukrani zake nyingi kwa familia ya Hayati Baba wa Taifa kwa kumkumbuka na kusherehekea naye kufikia umri huo.
Mzee KK akiwa nyumbani kwake muda mchache kabla ya kupokea salamu zake za pongezi kutoka kwa Mama Maria Nyerere.
Mzee KK akipokea zawadi aliyotunukiwa na Mama Maria Nyerere. Anaye mkabidhi zawadi hiyo ni motto wake Mhe. Makongoro Nyerere akishuhudiwa na Mhe. Balozi Grace Mujuma.
Mzee KK akiwa na zawadi yake ya Kinyago alichotunukiwa na Mama Maria Nyerere.
Mzee Kaunda akiwa kwenye picha ya pamoja na binti yake Catherine Kaunda, Mhe Makongoro Nyerere na Mhe Balozi Grace Mujuma.




No comments:
Post a Comment