Naibu wa kocha ya klabu ya
Chelsea, Rui Farai amepigwa marufuku ya kutokutenda jukumu lake uwajani
kama naibu wa kocha kwa jumla ya mechi sita na faini ya pauni £30,000 .
Mreno huyo alikirii makosa yake mawili ya kumkemea refa Mike Dean na kuzua vurumayi uwanjani na kupewa kadi nyekundu.
Marufuku hiyo ilijumlisha mechi mbili za nyumbani zilozobakia msimu huu dhidi klabu ya Norwich na Cardiff na nne katika msimu mpya .
Naye kocha mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho pia anakabiliana na makosa ya utovu wa nidhamu kwa kutumia kinaya kumkejeli na kumpongeza refa Mike Dean na msaidizi wake Mike Riley.
Haya yanajiri baada ya kiungo cha kati Ramires kupigwa marufuku kutoshiriki mechi nne kutokana na kitendo cha kumgonga kumbo mchezaji wa Sunderland Larsson wakati wa mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment