Mmoja kati ya marehemu aliyepatwa na janga hilo.
KUFUATIA vifo vya watoto watatu waliokufa kwa pamoja ndani ya bwawa la kuogelea ‘swimming pool’ kwenye Hoteli ya Landmark, Mbezi Beach jijini Dar, undani wa vifo hivyo umejulikana, Amani lina kisa kamili.
CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, watoto walionusurika kufa ambao walikuwa
wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwenzao ‘bethidei’ aliyejulikana kwa
jina la Derrick Mboka, waliwaona marehemu wakielea kwenye maji ya bwawa
hilo walilosema kuwa ni la kuogelea watu wazima.
Chanzo
kiliendelea kuweka wazi kwamba baada ya kuwaona wenzao wakielea, watoto
hao walipiga kelele jambo lililowashtua walinzi wa hoteli hiyo upande
wa bwawa ambao walifika haraka kuwatoa marehemu wakiwa tayari
wameshafariki dunia huku mtoto mmoja akihangaika kujiokoa.
No comments:
Post a Comment