Wednesday, May 7, 2014

PICHA KAMILI ZA TAMASHA LA PASAKA KUTOKA MWANZA, MALOPE AMALIZA

Malkia wa nyimbo za injili barani Afrika, Rebecca Malope.
Kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye hitimisho la Pasaka, basi fursa ipo kupitia hapa kuona namna matukio yote yalivyokuwa, ambapo muimbaji mkongwe wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini - tena malkia wa nyimbo za injili barani Afrika, Rebecca Malope alifanikiwa kugusa mioyo ya watu, si tu kwa uimbaji, bali hata kupitia kwa kuwatia moyo kwamba Mungu anasikia pale umuombapo.

Sehemu ya watu waliokuwa wakiingia uwanjani hapo.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake.
Son of Tanzania, Ephraim Sekeleti kutoka Zambia
Katika tamasha hilo ambalo lilihudumiiuwa na waimbaji mbalimbali kutoka maeneo tofauti barani Afrika, lilikuwa na ugeni rasmi wa Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, ambapo alisisitiza watu kuliombea taifa katika mchakato huu mgumu ambao unapitia wa kupata katiba. Na pia wakati hupohuo risala iliyosomwa kwa mgeni huyo rasmi na mojawapo wa waratibu wa tamasha hilo, Bwana John Melele, Mhe. Ngeleja ametakiwa kuwakumbusha wabunge wenzake kuwa pasipo Mungu hakuna kitakachowezekana, na hivyo wamtangulize.
BWANA asifiweeee, asema mgeni rasmi, mbunge wa jimbo la Sengerema, Mheshimiwa William Ngeleja.
Tukio la uzinduzi wa album ya muimbaji Grace pia lilifanyika ambapo mgeni rasmi alikiri wazi kuwa amani ya Tanzania pia inachangiwa na waimbaji wa nyimbo za injili, na hivyo wanatakiwa kusonga mbele bila kukata tamaa.

Wachungaji wakiwa wameiwekea mikono album ya mwanadada Grace Mwikabwe
Rebecca Malope na timu yake wakiingia ndani ya uwanja tayari kwa kuhudumu.
Akipokulewa na baadhi ya waimbaji wenzake.
Timu ikiwa 'standby'
Sasa tayari kwa kazi


Look at me...

Kila mkono na ukawa bize usipitwe, shida sasa mtu akipiga hapo, aarrgh.

enhe
Nyumbani tunamchezea Mungu namna hii.





Boniphace: uko tayari kuimba? Ephraim: Hebu nitazame katika picha zijazo utapata jibu lako.

Mgeni rasmi
Mgeni rasmi akizindua album ya Grace.
Mkurugeni wa Msama Promotions, Alex Msama akiongea jambo kwa umma.
Risala ikisomwa kwa mgeni rasmi
John Lisu na timu yake.


Huku chini nako kazi na dawa.



Edson Zako Mwasabwite akiwa na Rebecca Malope na Silas Mbise wa Team GK.


Edson Mwasabwite, ambaye amenusurika ajali hivi karibuni, ni kwa Neema tu.
Upendo Nkone na timu yake

Wakijongea kwenye madhabahu
Kama mawimbiii
Upendo wa Yesu wamzunguka, na hata watu pia.
haachi mtu kitu hapa.
hata ufanyeje
"Hahaha, umenigusa aisee, hadi nimecheza" Alex Msama akifurahia jambo na Sarah K.





Mess Jacob Chengula
The Voice Acapella.

Baadhi ya wachungaji wakati wakiingia uwanjani

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake