 |
| Malkia wa nyimbo za injili barani Afrika, Rebecca Malope. |
Kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza kwenye hitimisho la Pasaka, basi fursa ipo kupitia hapa kuona
namna matukio yote yalivyokuwa, ambapo muimbaji mkongwe wa nyimbo za
injili kutoka Afrika Kusini - tena malkia wa nyimbo za injili barani
Afrika, Rebecca Malope alifanikiwa kugusa mioyo ya watu, si tu kwa
uimbaji, bali hata kupitia kwa kuwatia moyo kwamba Mungu anasikia pale
umuombapo.
 |
| Sehemu ya watu waliokuwa wakiingia uwanjani hapo. |
 |
| Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake. |
 |
| Son of Tanzania, Ephraim Sekeleti kutoka Zambia |
Katika tamasha hilo ambalo lilihudumiiuwa na waimbaji mbalimbali kutoka
maeneo tofauti barani Afrika, lilikuwa na ugeni rasmi wa Mbunge wa jimbo
la Sengerema, William Ngeleja, ambapo alisisitiza watu kuliombea taifa
katika mchakato huu mgumu ambao unapitia wa kupata katiba. Na pia wakati
hupohuo risala iliyosomwa kwa mgeni huyo rasmi na mojawapo wa waratibu
wa tamasha hilo, Bwana John Melele, Mhe. Ngeleja ametakiwa kuwakumbusha
wabunge wenzake kuwa pasipo Mungu hakuna kitakachowezekana, na hivyo
wamtangulize.
 |
| BWANA asifiweeee, asema mgeni rasmi, mbunge wa jimbo la Sengerema, Mheshimiwa William Ngeleja. |
Tukio la uzinduzi wa album ya muimbaji Grace pia lilifanyika ambapo
mgeni rasmi alikiri wazi kuwa amani ya Tanzania pia inachangiwa na
waimbaji wa nyimbo za injili, na hivyo wanatakiwa kusonga mbele bila
kukata tamaa.
 |
| Wachungaji wakiwa wameiwekea mikono album ya mwanadada Grace Mwikabwe |
 |
| Rebecca Malope na timu yake wakiingia ndani ya uwanja tayari kwa kuhudumu. |
 |
| Akipokulewa na baadhi ya waimbaji wenzake. |
 |
| Timu ikiwa 'standby' |
 |
| Sasa tayari kwa kazi |
 |
| Look at me... |
 |
| Kila mkono na ukawa bize usipitwe, shida sasa mtu akipiga hapo, aarrgh. |
 |
| enhe |
 |
| Nyumbani tunamchezea Mungu namna hii. |
 |
| Boniphace: uko tayari kuimba? Ephraim: Hebu nitazame katika picha zijazo utapata jibu lako. |
Mgeni rasmi
 |
| Mgeni rasmi akizindua album ya Grace. |
 |
| Mkurugeni wa Msama Promotions, Alex Msama akiongea jambo kwa umma. |
 |
| Risala ikisomwa kwa mgeni rasmi |
John Lisu na timu yake.
Huku chini nako kazi na dawa.
 |
| Edson Zako Mwasabwite akiwa na Rebecca Malope na Silas Mbise wa Team GK. |
Upendo Nkone na timu yake
 |
| Wakijongea kwenye madhabahu |
 |
| Kama mawimbiii |
 |
| Upendo wa Yesu wamzunguka, na hata watu pia. |
 |
| haachi mtu kitu hapa. |
 |
| hata ufanyeje |
 |
| "Hahaha, umenigusa aisee, hadi nimecheza" Alex Msama akifurahia jambo na Sarah K. |
 |
| Mess Jacob Chengula |
 |
| The Voice Acapella. |
 |
| Baadhi ya wachungaji wakati wakiingia uwanjani |
No comments:
Post a Comment