Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametoa salamu za rambirambi na pole nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya
Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan na wananchi wa Nigeria kufuatia
mfululizo wa vitendo vya ugaidi ambavyo vimepoteza maisha ya maelefu ya
wananchi wa nchi hiyo na kutekwa nyara kwa mamia ya watu wakiwemo
wanafunzi wa kike wa sekondari.
Katika salamu zake za pole kwa Rais Jonathan, Rais Kikwete amesema: “Napenda
kutoa salamu za rambirambi na pole zetu nyingi kwako Mheshimiwa Rais na
wananchi wa Nigeria kufuatia mfululizo wa vitendo vya kigaidi ambavyo
vimepoteza maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo na wengine kutekwa
nyara. Tumekuja kuonyesha mshikamano wetu na wananchi wa Nigeria.”
Rais
Kikwete ametoa pole hizo mwanzoni mwa hotuba yake kwenye mkutano wa
marais uliozungumzia umuhimu wa miundombinu ya kimkakati katika Afrika
ikiwa ni sehemu ya Kongamano la Uchumi Duniani (WEF) Afrika kwenye
Hoteli ya Transcorp Hilton mjini Abuja, Nigeria.
Akizungumza mbele ya Rais Jonathan na viongozi wengine wa Afrika, Rais Kikwete amemwambia kiongozi huyo wa Nigeria:“Tulishauriwa
sana tusije kuhudhuria kongamano hili kwa sababu ya hali ya usalama.
Lakini tusingefika tungewapa ushindi magaidi hawa ambao wanasumbua
sehemu kubwa ya Bara letu. Mheshimiwa Rais sala zetu ziko nawe na
wananchi wa Nigeria katika kipindi hiki kigumu.”
Serikali
ya Nigeria imekuwa inapambana na vikundi vya kigaidi na hasa kile cha
Boko Haram ambacho kimekuwa kinaendesha kila aina ya ugaidi hasa katika
maeneo ya kaskazini ya nchi hiyo.
Wiki
tatu zilizopita, kikundi hicho ambacho lengo lake kuu ni kupinga elimu
ya magharibi kiliteka watoto zaidi ya 200 wa kike kutoka mabweni ya
shule moja ya sekondari kaskazini mwa nchi hiyo.
Mpaka
sasa watoto hao hawajapatikana, jambo ambalo linaipa shinikizo kubwa
Serikali ya Nigeria. Boko Haram kimetishia kuwauza sokoni watoto hao wa
kike.
Siku
mbili zilizopta, kikundi hicho kiliteka nyara watu wengine wanane na
usiku wa jana, kimeua watu wanaokadiriwa kufikia 300 katika vijiji mbali
mbali vya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8 Mei, 2014

No comments:
Post a Comment