
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA
--
Ndugu
waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ifuatayo ni taarifa
ya tukio moja la kifo na taarifa ya Operesheni inayoendelea katika
wilaya zote za mkoa wa Tabora. Ambapo kufuatia operesheni hizo
tulifanikiwa kukamata watuhumiwa wa makosa mbali mbali kama ifuatavyo:-
Mnamo
tarehe 04.05.2014 majira ya saa 10:00hrs huko eneo la Utwigu wilaya ya
Nzega FRANCE S/O AMBROSE HUSSEIN 11yrs, Mnyamwezi mwanafunzi wa darasa
la Tano katika shule ya Msingi Mwanhala alifariki dunia baada ya
kutumbukia katika bwawa la maji ambapo alikuwa ameenda kwa ajili ya
kuogelea.
Tarehe
01.05.2014 huko wilaya ya Nzega alikamatwa FROLA D/O SHIJA, 28yrs,
mnyamwezi, mkulima na mkazi wa kujiji cha Igalula akiwa na bunduki aina
ya Gobore ambayo anamiliki kinyume na sheria. Mtuhumiwa amefikishwa
mahakamani.
Aidha
tarehe 02.05.2014 huko katika eneo la Utwigu kata ya Nyasa wilaya ya
Nzega walikamatwa SHIJA S/O KAPONA, 39yrs, Mnyamwezi, Mkulima na BAHATI
S/O SHIJA, 28yrs, wote wakazi wa Utwigu wakiwa na vipodozi aina ya Lemon
Vate Cream 02, Beater Soap 02, Deproson chupa 15, Demason 01, na
Banistar 01, vipodozi hivyo vilibainika kuwa havifai kwa matumizi ya
binadamu na mtaalam kutoka TFDA. Watuhumiwa wote wamefikishwa
mahakamani.
Katika
opereheni hii pia wamekamatwa PILI D/O BUNDALA 65yrs, Mnyamwezi,
MACHIBYA S/O MGETE 40 yrs, Mnyamwezi, KULWA S/O MASANJA, 35yrs, Msukuma,
DAUDI S/O KABOGA 28yrs, Msukuma, MWAJUMA D/O RAJABU, 30yrs, Mnyamwezi,
na MWASITI D/O MUHOJA 37yrs, wote wakazi wa kata ya Nyasa – Nzega wakiwa
na Pombe ya moshi lita 15, pia watuhumiwa wote hawa ni watumiaji na
wauzaji wa pombe hiyo haramu. Wote wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Jeshi
la Polisi linazidi wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi
lao ili kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua
wahalifu, aidha wazazi napenda kuwakumbusha wazazi kuwaangalia watoto na
kuwafuatilia katika michezo yao ya kila siku, pia napenda kuwaasa
wananchi kufuata sheria za nchi na pia kwa wale wote ambao wanamiliki
magobore kinyume na sheria wasalimishe magobore hayo kwa kuwa
operessheni hii ni endelevu.
Imetolewa na :-
SUZAN KAGANDA – ACP
KAMANDA WA POLIS
MKOA WA TABORA.
No comments:
Post a Comment