Advertisements

Saturday, May 10, 2014

Safari ya Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki kuelekea Tanzania 
Michango kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba wa Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki aliyefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 April 2014 imekamilika. Mpaka sasa kiasi cha dolla 20,000 kimepatikana kama ifuatavyo:
·      Watanzania Marekani wametoa dolla 5,300
·      Familia, ndugu na Jamaa wa Tanzania wametoa dolla 11,000
·      Watoto wa Marehemu Erick na Mary Kagaruki wametoa kiasi kilichobakia cha dolla 3,700.
 
Watoto wa Marehemu Erick Kagaruki na Mary Kagaruki na familia nzima ya Marehemu mama Harriette Peace Kagaruki wanapenda kuwashukuru wote mliotoa michango, rambirambi na mliofanikisha kwa namna moja au nyingine shughuli hizi za msiba ziweze kufanikiwa.
 
Shukrani nyingine ziende kwa Watanzania wote na rafiki wa Watanzania waliochangia shughuli za msiba huu hapa Marekani na Tanzania.
 
Mwili wa Marehemu umeshaletwa New Jersey kutoka Philadelphia tayari kupelekwa Tanzania siku ya Jumanne usiku saa tatu kupitia airport ya Newark na British Airways via Entebbe.
 
Mwili utawasili Entebbe Jumatano kabla ya safari ya kuelekea Bukoba kuanza kwa ajili ya shughuli mazishi kuanza.
 
Familia inapenda tena kuwashukuru wote kwa kufanikisha michango na shughuli za sasa za msiba huu. Tunawaomba Watanzania wote tuendelee kushirikiana katika nyakati za shida na raha kama tulivyoshirikiana wakati huu wa msiba.
 
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Byabusha – 914-584-7502
  
 
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
 
Deogratius Mhella, Katibu New York Tanzanian Community.

3 comments:

Anonymous said...

INASIKITISHA JAMANI WATANZANIA TUMCHANGIYENI JAMANI ANATESEKA MAMA WA WATU ANATAKA AKAPUMZIKE KWENYE MCHANGA WA NYUMBANI.

Anonymous said...

poleni wafiwa. mie nishachanga, ila huwa sielewi mbona bei za usafirishaji huwa zinatofautiona sana. utasikia $12,000 au $15,000 au hiyo $20,000 etc. who decides how much ni airline au hizo ni standard bei. i am just curious ili nijue ni kiasi gani ni-jisevie for me

Anonymous said...

kusafirisha mwili kwenda Tanzania si $20,000. Waulizeni wazoefu viongozi DMV watawasaidia kuwapa mawazo ya kupunguza bei