ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 3, 2014

TANGAZO LA SHUKRAN

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shina CCM Maryland, Ndugu Mrisho Mzese, Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Ndugu Mwigulu Nchemaba na Katibu wa Shina CCM Marland ndugu Marco Mbullu

Uongozi wa shina la CCM Maryland unapenda kutoa shukran za dhati kwa naibu katibu mkuu CCM bara ndugu Mwigulu Nchemba pamoja wanachama na wapenzi wote wa CCM pamoja na watanzania wote walioweza kushiriki katika sherehe za uzinduzi wa shina letu la CCM Maryland.

Uongozi wa shina umethamini na kuutambua mchango huo mkubwa. Tunaomba tuendelee na moyo huo huo sisi kama watanzania. Sisi ni watanzania kwanza! 

(TANGAZO LIMETOLEWA NA UONGOZI WA SHINA) 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi

3 comments:

Anonymous said...

Hivi nyinyi wa shina la german town ndio mnajitoa akili au? Mwenyekiti wenu analazimisha cheo. Wacheni kudanganya watu ... Kama viongozi acheni upotofu. Na dj luke sio unajitolea tu uwe unapima sasa na shina la hyattsville na wao wajiitaje? Mrisho kua bwana acheni kujidhalilisha. Luke usibanie

Anonymous said...

Hongereni sana wangugu. Wengi wetu tunafahamu kuwa hapa DMV tayari kuba tawi la CCM ambalo mwenyekiti wake ni George Sebo. Kwavile kuna tawi na shina, kati ya mwenyekiti wa tawi na yule wa shina nani ni bosi??????????

Anonymous said...

Naona sasa mumeishiwa. Mpaka lini haya masuala ya CCM ughaibuni? Mimi kama mwanachama wa CCM siipendi kabisa hii idea ya kufunguwa mashina ya CCM huku ni kuwapa nafasi wapinzani wetu watuone sisi tumeishiwa na sera. Mwigulu Nchemba tumia nafasi yakonkama yako kama Naibu Waziri na sio mshereheshaji wa sera za chama.