Saturday, May 31, 2014

UZINDUZI RASMI WA KADI MPYA WAFANYIKA

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (kushoto) akipokea hati ya makubaliano kutoka kwa Mkurugenzi wa TPB Bw Sabasaba Moshingi (kulia) katikati ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Bw Juma Nkamia wakati wa Uzinduzi wa Kadi Mpya za ATM za Wanachama
Shirika la Benki ya Postay nchini (TPB) na klabu ya Young Africans leo wamezindua rasmi kadi mpya za wanachama zenye mfumo wa Kielektoniki (ATM) ambazo zitaanza kutumika mwezi Juni mwaka huu kwenye sherehe zilizofanyika katlika Hoteli ya Hyatt (Zamani Kempsink) eneo la Posta jijini Dar es salaam.
Sherehe hizo za uzinduzi wa kadi mpya za wanachama zilifanya na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Bw Juma Nkamia ambaye aliipongeza Benki ya Posta na vilabu vya Simba na Yanga kwa hatua nzuri waliofikia ya kisasa ya kuongeza wanachama na kujikomboa kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta nchini Bw Sabasaba Moshingi alisema wao kama Benki ya kizalendo wameamua kuanza na vilabu viwili vyenye wapenzi na wanchama wengi kwa ajili ya kuvisaidia kuwafikia watu wao nchini kote na kongeza pato la vilabu vyao kwa kulipia ada zao kupitia Benki ya Posta.

"Benki yetu ina matawi nchini kote, hivyo kwa sasa watu wanaopenda kuwa wanachama wa Yanga na walikua wanashindwa kufika makao makuu kupata kadi zao, njia imekua rahisi wanaweza fika kwenye matawi yetu nchi nzima na wakajiandaikisha kisha baadae kupewa kadi zao za uanachama zenye mfumo wa ATM ambazo pia wataweza kuzitumia katika shuguli zingine za Kibenki, kuweka, kutoa kwenye mashine za Umoja Switch nchi nzima" alisema Sabasaba. 

Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw Clement Sanga alisema wanaishukuru Benki ya Posta kwa kukubali kufanya kazi hiyo ya kuandikisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kisasa jambo ambalo litapelekea kuongeza idadi ya wanachama kwa urahisi na kuongeza pato la klabu.

Aidha Sanga alisema kwa mfumo huu mpya ni rahisi kujua wanachama walio hai kwa kuwa kutakua na kumbukumbu zote kwenye mtandao ambapo wamanachama asiye hai kadi yake haitakua na uwezo wa kusoma kwenye mashine wala kupata huduma zozote za Kibenki.

Beki ya Posta na matawi yake kote nchini wanatarajia kuanza zoezi la kuandikisha wanachama kwenye mfumo mpya wa ATM Card mwezi Juni mwaka huu.

No comments: