ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 12, 2014

Wanafunzi waandamana baada ya mwenzao kufa; Mwalimu Mkuu azimia

Fikra inataarifu kuwa Wanafunzi wapatao 344 wa shule ya sekondari ya wasichana Masasi mkoani Mtwara wameandamana hadi nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Masasi, Farida Mgomi wakishinikiza kuondolewa kwa mkuu wa shule hiyo, Reinader Tesha kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha tano Omega Kabuje aliyefariki jana (Jumamosi).

Maandamano hayo yameganywa leo, Jumapili saa 11 alfajiri lakini wanafunzi hao hawakufanikiwa kukutana na Mgomi kwa kuwa alikuwa safarini Mtwara.

Mkuu wa shule hiyo, Reinader Tesha alijikuta akipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Masasi ya Mkomaindo ambapo anaendelea kupata matibabu baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake alikokuwa amejifungia kwa takribani saa nne.
Hatua ya wanafunzi hao ambayo imekuja wakati tume iliyoundwa na baraza la madiwani kuchunguza malalamiko yanayomhusu mkuu wa shule hiyo jinsi anavyowanyanyasa wananfunzi wake na utendaji wake wa kazi hasa tuhuma za manyanyaso yanyofanyiwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Dada mkuu wa shule hiyo, Regina Christopher alibainisha kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na vitendo vya mkuu huyo ambapo mara zote amekuwa anawanyanyasa na kutowathamini pindi wanapokuwa wagonjwa na walimu wa kutowajali wanafunzi.

Alidai kuwa mkuu huyo wa shule amekuwa hafuatilii wanapougua ambapo jukumu linakuwa la wanafunzi wenyewe kutafuta usafiri wa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kupata matibabu kwani shule haijishughulishi na huduma za matibabu.

“Mwenzetu amefariki leo na hii tunajua si kwa mipango ya Mungu bali kuna uzembe wa walimu na watoa huduma hivyo tumeamua leo kuandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya kuonesha kukerwa na tabia hizo,” alisema Regina. ...Habari hii inaendelea hapa ...Fikra Pevu.

No comments: