Wadau wahoji analinda maslahi ya nani?
Atapuuza kilio cha Watanzania hadi lini?
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameshambuliwa vikali kutokana na kauli zake za kila mara za kuwadhihaki na kuwadharau Watanzania kwamba hawana uwezo wa kuwekeza katika sekta ya gesi bali kufanya biashara ya kuuza juisi.
Waziri Muhongo pia amekosolewa kwa kauli yake kwamba Watanzania wazawa wanaolalamika kutopewa kipaumbele katika biashara hiyo ni wezi na wababaishaji.
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amesema atathibitisha uongo wa Muhongo, kuwa Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi wakati atakapowasilisha hotuba yake ya bajeti bungeni.
Kadhalika, ametoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete, kusitisha zabuni inayokaribia kufunguliwa ya kunadi vitalu vya gesi kwa kuwa ni lazima kuwe na sheria mpya ya gesi na kufanya mabadiliko ya sheria ya mafuta ya mwaka 1980 iliyopitwa na wakati, sera ya gesi yenye sura pana.
“Uongo mkubwa ni kusema Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye vitalu vya gesi bali wanaweza kuendesha biashara ya juisi, uongo mwingine ni eti tukichelewa kuvuna wenzetu wa Msumbuji watawahi na Watanzania watakuwa tumepoteza fursa...anafanya gesi kama ndizi au nyanya ambazo zinaweza kuoza iwapo zitachelewa kuvunwa, kuna uongo mwingi na nitauweka bayana kwenye hotuba yangu.
“Waziri Muhongo alijibu kwa wepesi kuwa hafanyi kazi magazetini kana kwamba jambo nililolokuwa nazungumzia limetolewa na magazeti...tusubiri kwenye bajeti yangu nitaweka bayana mambo mengi,” alifafanua.
Mnyika alisema sera ya gesi iliyopo ina kasoro kubwa sana, kwa kuwa iliyopo sasa haihusiki na ngazi zote kuanzia chini hadi juu na kwamba ni dhaifu.
DK. BISIMBA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba alisema kauli za Prof. Muhongo si za kizalendo na zinawavunja moyo Watanzania.
“Sijui ni Mtanzania wa wapi ambaye hana uzalendo wa kuonyesha kuwatia moyo Watanzania wenzake ambao wana nia ya kuwekeza na hii si mara yake ya kwanza kutoa kauli kama hizi za kuwakatisha tamaa Watanzania badala ya kutoa kipaumbele kwao, yeye anatoa kauli ambazo si nzuri,” alisema na kuongeza:
“Hii ni tofauti na nchi za wenzetu, viongozi huwatia moyo wananchi wao, lakini Watanzania walio wengi hatupendi vya kwetu bali vya wenzetu, tunakatishana tamaa wenyewe. Kwa kweli tumechoka na kauli kama hizi ambazo zinatolewa na kiongozi mkubwa serikalini.”
DK. BENSON BANA
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema: “Kauli zilizotolewa na Prof. Muhongo kwa mwanasiasa hazifai kwa sababau yeye ni kiongozi wa serikali na ukiangalia malengo ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta) ya mwaka 2005, yanalenga kuwaondolea umaskini wananchi ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika mambo kama haya ya uendeshaji wa shughuli za rasilimali zao zinazopatikana nchini.
“Pamoja na kuiheshimu elimu yake, kauli zake hazifai. Malengo yetu tangu Uhuru ni kuona kwamba wananchi wanashirikishwa vya kutosha katika shughuli zote za kimaendeleo na uchumi. Wazawa wanawezeshwa hata kama wataingia ubia na watu wa kutoka nje. Waziri huyu anaonekana hajasoma vizuri somo la mawasiliano ya umma na kitendo cha kuwaita Watanzania wenzake wezi basi hata yeye ni mwizi,” alisema Dk. Bana.
“Nafikiri anahitaji kwenda shule ili afahamu lugha ya kuwasiliana na wananchi, ni vyema akaacha tabia ya kuwabeza Watanzania, yeye anatakiwa kuangalia jinsi ya kuwasaidia Watanzania kwa kuwapa mitaji, kwani uwezo hauji mara moja bali ni kwa kuwezeshwa,” alisema Dk. Bana.
MBOWE
Kuandamwa kwa Profesa Muhongo, kunaongezwa nguvu baada ya kushutumiwa vikali na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wakati akitoa bajeti mbadala ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni wiki iliyopita.
Mbowe alimtaja Waziri Muhongo kama kilelezo cha viongozi wa umma wanaokashifu, kuwapuuza na kuwakatisha tamaa wawekezaji wazawa ili wasihimili uchumi wa taifa lao.
Alisema serikali inapuuza wawekezaji wa ndani kwa kuwapa kipaumbele wa nje kwa madai wana mitaji mikubwa na kupuuza wazawa huku wa nje wakigeuza rasilimali za nchi kama njia ya kujipatia mikopo.
Alisema Waziri Muhongo bila woga anasisitiza kuwa wawekezaji wa nje wanaaminika na serikali hutafuta mitaji toka taasisi za fedha za kwao na kimataifa baada ya kupewa vibali vya kuvunja rasilimali za Tanzania kwa bei ya kutupa.
“Inasikitisha kusikia kauli za viongozi waandamizi wa serikali zinazovunja moyo wawekezaji wa ndani badala ya serikali kuwa chombo cha uwekezaji wa wazawa…inawakashifu, kudharau na kuwadhalilisha,” alifafanua Mbowe.
Alisema kauli ya Prof. Muhongo, ilitakiwa kukemewa na serikali, lakini imekaa kimya.
Alisema siyo kukemewa pekee bali Waziri huyo alipaswa kuwajibishwa moja kwa moja kwa kujiuzulu au kufukuzwa kazi, lakini cha kushangaza, viongozi wakuu wa serikali walikaa kimya na wengine kushangilia.
Mbowe alisema kutokana na kauli hiyo ni ushahidi tosha kuwa kauli kuwa sekta binafsi ni injini ya kukua kwa uchumi kwao inamaanisha sekta binafsi ya nje.
Alisema kauli za viongozi waandamizi hazitakiwi kufumbiwa macho na kuwapo katika utumishi wa umma.
Aidha, aliwataka Watanzania kutokata tamaa kuhusiana na uwezo wa Watanzania kushiriki moja kwa moja katika kuendeleza rasilimali na ifikie mahali pa kuaminishwa kuwa si dhambi kuwapendelea wazawa katika uwekezaji wa gesi na mafuta pamoja na kuandaa kizazi cha kesho cha wawekezaji wazawa.
Akichangia hotuba ya makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu wiki iliyopita, Waziri Muhonho mbali ya kueleza jinsi ilivyo vigumu kwa Watanzania kupata fedha za kufanya utafiti na uchimbaji wa gesi na petrol, alisema bei kubwa zilizowekwa ni mahususi za kwa ajili ya kuwaondoa wababaishaji na wezi; na kwamba ameanza mkakati w akuwanyang’anya wababaishaji na wezi vitalu vya madini kwa kuwa wamevihodhi bila kuviendeleza.
Imeandikwa na Salome Kitomari, Dodoma, Samson Fridolini na Christina Mwakangale, Dar.

CHANZO: NIPASHE

4 comments:
Kwani nchi haina rais? Mwongozo wa rais ni upi? Kama hakaripii labda amemtuma aseme hivyo.
raisi si chekacheka tu kila leo na wapo wanatumia udhaifu wake huu na kumpanda kichwaaa waulizeni watu wa dini makanisani watakuambiyeni mwongozo wa raisi ni upi
Manufaa ya kwanza ya mradi wowote ni watu wa daraja la chini kupatiwa elimu ya ku run miradi hiyo na si kwa watu wa daraja la juu kuhodhi vitalu na mwishowe kuvipangisha kwa wawekezaji. Mwekezaji wa nje anapokuja kuwekeza amewekewa tozo ambalo mwekezaji wa nyumbani atajaribu kulikwepa. hawa wanaodai wawekezaji ni madalali kati na huo ndio uchungu wao. Badala ya hayo wanayoyasema na kutuhumu, kuweka watu wa kuwasemea bungeni kwa malipo ya kufund chaguzi zao kwa nini wasiwasemee vijana na wananchi waliozaliwa na wanaoishi karibu na inapoanzishwa miradi ili wapate elimu ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi na kupata huduma muhimu za kijamii? Hawa ni watu muhimu kabisa na si madalali. Kumbukeni Ubepari ukianza kuyumba kuna watu wataitwa lobbiest na tukigusa huko basi Tanzania itauzwa na hatutakuwa hata na pakulalamikia.
Acheni kumpigia tarumbeta Mengi.Kabla hujaanza kumlaumu Waziri tafakari kwa makini miradi waliyoachiwa wazawa ie,Tanzanite etc.Hata katika miradi ambayo wazawa waliiomba kuindesha wameishia kuwaingiza wawekazi wa nje...na mwananchi wa kawaida hajafaidika lolote na uwekezaji wao.Kinachotakiwa ni kuwa na sera bora zitakazo simamia rasilimali period.
Post a Comment