Friday, May 30, 2014

ZIARA YA KINANA YALETA NEEMA MKOANI MANYARA

  • Serikali yakubali kuwaajiri wafanyakazi wa Hospitali ya Hydom
  • Imeongeza ruzuku kwa hospitali ya Hydom kutoka milioni 200 mpaka 320
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilya ya Babati Mjini ambapo aliwaambia wananchi wawe na ushirikiano katika shughuli za maendeleo yao na aliwaambia kuchapa kazi ndio njia pekee ya ukombozi katika kuleta maendeleo.
 Wananchi wa Babati mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye Uwanja wa Kwaraa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati mkubwa wa watu katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubiwa wakazi wa Babati Mjini ambapo aliwaambia wananchi wasihadaike na maneno ya upinzani kwani upinzani nchini unazidi kufa siku hadi siku .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Manyara ambapo alisisitiza viongozi kutoa elimu kwa wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya .
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Eng. Omari Chambo akitoa tamko la serikali la kuajiri watumishi wa hospitali ya Hydom ikiwa pamoja na Serikali kuongeza  ruzuku kwa hospitali hiyo kutoka milioni 200 mpaka milioni 320,Ongezeko hilo linatokana na ziara ya Katibu Mkuu wa CCM aliyofanya katika Hospitali ya Hydom siku ya tarehe 28 Mei 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua majengo ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Maabara ya hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara Dk. Daniel Mbwambo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya  maji Bi.Zena Rashid baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kata ya Bonga wilaya ya Babati mjini.Katika ziara yake ya wilaya ya Babati mjini Katibu Mkuu alitembelea miradi mingine ya ujenzi wa maabara, nyumba za walimu, kufungua mashina ya CCM pamoja na ujenzi wa ofisi za Tawi CCM.

1 comment:

Anonymous said...

NAPE yaani hakuna unachikijua zaidi ya kungangana na WAPINZANI WAPINZANI kwani wao sio wanasiasa!!?? hebu jaribu kuongealea mambo yanayowahusu wananchi na maendeleo yao utakuwa unaonekana mwanasiasa uliyekomaa!! hii ni aibu!!!!!!!!!