Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na
kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa
kushirikiana na serikali.Katibu Mkuu alisisitiza serikali kuchukua hatua
za haraka kwa wale wote waliojichukulia mali ya serikali bila utaratibu
hasa nyumba za madaktari.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na
kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera
zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa
hilo kiasi cha kurejea CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakijiji cha
Bashei ambao walimueleza kuwa wanalima sana kitunguu saumu lakini soko
si zuri na kumuomba awasaidie kutafuta soko la kdumu, tatizo jingine ni ucheleweshaji wa kujenga bwawa la maji, Katika ziara hizi za Katibu
Mkuu wananchi wamekuwa na imani kubwa na CCM kwa ushirikiano wanaoupata
kwani majibu ya maswali yao yanakuwa ya kuridhisha.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa
Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini
ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya
alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa
migogoro ya wakulima na wafugaji ,pili atafanya jitihada za dhati
kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye
masuala ya ardhi.
Diwani wa Kata ya Eshkesh kutoka chama cha CUF Ndugu Naftal Z Kihandu akishukuru kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kuwasikiliza wananchi wa kata yake na kufungua njia kwa kuchangia mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Hydom na
kuwaambia wapunguze muda na mambo ya siasa ,watumie muda mwingi
kushikama na kujenga maendeleo yao.
Wananchi wa Hydom wakinyoosha mikono yao kuunga mkono jitihada za CCM katika kuleta maendeleo nchini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya Chadema
iliyorudishwa kwake na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema
(BAWACHA) Victoria Mshanga ambaye amjiunga rasmi na CCM kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika Hydom.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga picha ya wanakijiji cha
Eshkesh pamoja na Richard Mwaikenda maarufu kama Kamanda wa
Matukio,Wananchi wa Eshkesh wanashida ya maji na Zahanati ambapo maji
yatapatikana karibuni kutokana na mipango ya halmashauri lakini zahanati
pia itaanza kujengwa baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuhamasisha kwa kuanza
kuwachangia mabati na Simenti na halmashauri na wanakijiji hao
wataongezea nguvu kukamilisha.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi na wanafunzi
wa uuguzi wa Hospitali ya Hydom .Katibu Mkuu aliupongeza Uongozi pamoja
na Watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa katika
kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati wa ujenzi
wa daraja la Qorong'aida linalounganisha Kilimapunda na Kidarafa na
linategemewa kugharimu zaidi ya bilioni moja.
No comments:
Post a Comment