Mwandishi
na Msimamizi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog Joseph Mwaisango akiwa anashuhudia
Simu hizo Feki na ambazo ukiziangalia kama mzoefu utajua ni Original ,
Simu hizo ni kama Samsung Galaxy na zenginezo .
Akiendelea kumuuliza maswali Mchina huyo.
Jijini
Mbeya katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Soweto kumeibuka
biashara ya hawa wanaowaita wawekezaji wachina ambao wamevamia jiji na
kufanya biashara ya Simu bei poa ambazo kwa kuziangalia kwa macho
utasema ni Original na kumbe ni Feki, Simu hizo mbalimbali ambazo
ukizikuta dukani kabisa na zenye bei kali kuanzia milioni au Laki tisa
na zaidi wao wanauza laki tatu tuu, na watu wengi wamesha ingizwa mjini
bila kujua.
Swali
linakuja Je Serikalini wahusika wanalitambua hili linalo endelea na
kama ndio wanalijua je wamewachukulia hatua zipi na huu ndio uwekezaji?
Kuweni makini epukeni kutapeliwa!
1 comment:
Na watanzania wakienda china wanaleta fake
Post a Comment