Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Nishati Endelevu kwa Wote wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. John Ashe mara baada ya uzinduzi wa Mwongo wa Nishati kwa wote. Mhe. Waziri Muhongo anaonekana nyuma ya Katibu Mkuu
Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo akiwa na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote. Walioketi nyuma ni wasaizidi wa Waziri.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongo wa Nishati Endelevu kwa Wote (2014-2024), uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote ( SE4ALL)unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1000. Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu.
Sehemu wa washiriki wa mkutano wa Nishati Endelevu kwa wote wakifuatilia uzinduzi wa Mwongo wa Nishati kwa wote .
Na Mwandishi Maalum
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki
Moon, jana alhamisi amezindua rasmi mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) wakati wa mkutano
unaohudhuriwa na wajumbe zaidi wa
1,000 wakiwamo zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati
20 wafanyabishara, mashirika ya kimataifa yakiwamo ya fedha
na Asasi zisizokuwa za kiserikali,
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Mkutano huu ambao ni ulioanza Juni 4 na utamalizika Juni 6, unaongozwa
na Waziri wa Nishani na Madini Professor Sospeter Muhongo ( Mb) ambaye pamoja na
kuhudhuria na kuchangia mijadala
mbalimbali, ijumaa ( June 6), atazungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu
nafasi ya Nishati katika Ajenda
za Maendeleo Endelevu baada ya
2015.
Akizindua mwongo huo Ban
ki Moon, pamoja na mambo mengine alieleza kuwa licha ya
kuwa pamoja suala la Nishati
ni suala la kidunia, lakini katika maeneo
mengi ni suala linalomhusu mwanamke zaidi.
“ Ni suala linalomhusu mwanamke zaidi, linaweza
kumaanisha tofauti kati ya usalama na hofu, uhuru na utumwa , hata
uhai na kifo. Dunia lazima ije
pamoja kumaliza umaskini wa nishati na
kuhakikisha watu maskini wanaweza kuhimili maisha yao na kustawi kiuchumi”
akasema Katibu Mkuu.
Akaongeza kuwa mpango wa nishati endelevu kwa wote zimeanza kuzaa matunda na kwamba ahadi za mabilioni ya dola zilizoahidiwa zimetolewa. Huku nchi zinazoendelea zaidi ya 80 zimejiunga na mpango huo.
Pamoja na
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kuzungumza wakati wa uzinduzi wa mwongo
huo, wengine waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Rais wa Iceland,
Olafur Ragnar Grimsson, Bw. John
Ashe,Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa na Rais wa Banki ya Dunia Jim Yong Kim ( kupitia
video) .
Mkutano huu
utafanya tathmini ya matokeo ahadi za mabilioni ya dola kuhusu upatiakani wa nishati, ufanisi wake na
nishati mbadala zilizoahidiwa wafanyabiashara, wawekezaji na watu wengine
walizotoa wakati wa Mkutano wa Maendeleo Endelevu ( Rio+20) uliofanyika mwaka
2012.
Aidha unatarajiwa kuhamasisha upatikanaji wa raslimali fedha, uwezeshaji na mipango ya
kufikia malengo ya nishati endelevu kwa wote.

No comments:
Post a Comment