ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 21, 2014

Chelsea wanauza watano

Wamo Lukaku, Demba Ba
20140402-155822.jpg
Chelsea wamekuwa wakijishughulisha sana na madirisha ya usajili, na msimu huu tayari wameshafanya kazi.

Wamemuuza beki wao David Luiz huko Paris Saint-Germain kwa kitita cha pauni milioni £50 na kumsajili kiungo wa Hispania, Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwa pauni milioni 30.

Biashara haijaisha na bado Jose Mourinho anataka kuuza wachezaji wengine wa timu ya kwanza.
Winga Marko Marin (25) aliyesajiliwa Stamford kutoka Werder Bremen ya Ujerumani kwa pauni milioni saba amekuwa na wakati mgumu hapo tangu asajiliwe mkiaka miwili iliyopita kabla ya kupelekwa kwa mkopo Sevilla ya Hispania.

Amecheza mechi sita tu za Ligi Kuu kwa Chelsea, sasa wanamuuza na Wolfsburg wameandaa pauni hizo hizo milioni saba kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani.

Romelu Lukaku ni mchezaji mzuri, mwenye nguvu, kasi, akili na anayefunga mabao mengi lakini haieleweki kwa nini Mourinho hampendi na amekuwa akimtoa kwa mkopo tu wakati hana washambuliaji wa kuaminika.

Lukaku (21) safari hii amewekewa bei ya pauni milioni 30 hivi ili auzwe ama Atletico Madrid au Juventus baada ya kucheza kwa mafanikio akiwa kwa mkopoWest Bromwich Albion na Everton.
Yupo Brazil na Timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Fernando Torres amekaa Chelsea bila mafanikio, baada ya kuwa amenunuliwa kwa rekodi kubwa zaidi klabuni hapo ya pauni milioni 50 Januari 2011.

Makocha na mbinu tofauti zimetumika kumfufua lakini ameshindwa ‘kuwaka’.
Hivi sasa Chelsea wanataka kumuuza na inasemekana Atletico Madrid wanamtaka.

Torres (30) ana kila dalili ya kurudi kwao Hispania, kwani Valencia nao wanahusishwa naye lakini bei yake lazima itakuwa imeshuka kutokana na umri mkubwa na ufanisi mdogo mbele ya lango.

Demba Ba ni mchezaji mwingine anayeonekana kama garasa, ambapo tangu aondoke Newcastle alikokuwa anawika sana, ameshindwa kukata kiu ya The Blues na anaonekana hana nafasi Stamford Bridge. Amefunga mabao 17 tu katika mechi 51.

Ba (29) alisajiliwa kwa pauni milioni saba Januari mwaka jana na sasa anauzwa kwa bei ambayo haijatajwa, kwani Mourinho akimpata Diego Costa wa Atletico, atamtafutia mshirika mwingine si hao waliokuwapo kama Samuel Eto’o aliyemaliza mkataba na hawa wengine.

Mournho pia anataka kumuuza Mwingereza anayechezea timu ya taifa, Ryan Bertrand (24) ambaye amekuwa hapo tangu 2005.

Beki huyu wa kushoto amecheza mechi 28 tu kwa Chelsea na alishatolewa kwa mkopo katika klabu sita tofauti na sasa Hull City wanataka kumnunua kwa pauni milioni 5.25.

Tanzania Sports

No comments: