Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akitoka ukumbi wa mkutano mara
baada ya kumaliza mazungumzo na madereza na wamiliki wa daladala
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amewomba Madereva na Wamiliki wa Daladala
zinazofanya safari kati ya Uyole na Sokomatola kuacha mgomo na kuendelea
kutoa huduma ya usafiri wakati Mamlaka husika zikishughulika suala lao.
Kauli
hiyo imekuja kufuatia mgomo wa siku mbili baada ya Daladala kugoma na kusitisha
huduma za usafiri kwa kile walichodai kuburuzwa na Watumishi wa Halmashauri ya
Jiji ,Polisi na Sumatra kwa kuwapangia njia ambayo imewasababishia umbali
mreffu na kuongeza gharama za uendeshaji na kuwatia hasara kubwa.
Kamanda
Msangi aliitoa kauli hiyo kufuatia kikao kilichoitshwa na Mlezi wa Daladala
njia ya Uyole Mchungaji William Mwamalanga kikao kilichofanyika katika ukumbi
wa Tumaini uliopo Ilomba Jijini Mbeya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
Madereva ambayo hayapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na Mamlaka hizo.
Msangi
amesema kitendo cha kugoma kutoa ni kutesa wananchi ambao hawana hatia hivyo
kuleta usumbufu usio wa lazima kwa Mamlaka husika zimepokea madai yao na
kuahidi kuyafanyia kazi ndani ya siku mbili na kuyatolea maamuzi ambayo
yataleta tija kwa pande zote.
Hata
hivyo Kamanda alipokea malalamiko kutoka kwa madereva kuhusu Askari wa Kikosi
cha Usalama barabarani na kuahidi kuyafanyia kazi na hatasita kuchukua hatua
endapo atabaini malalamiko yao yana msingi kama alivyochukua hatua hivi ya
kuwafukuza Askari sita waliotuhumiwa kwa kupokea rushwa barabarani.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Daladala Kanda ya Uyole Sunday Mwansasu amesema kuwa
kitendo kilichofanywa na Halmashauri ya Jiji na Sumatra cha kuwapangia njia
ambayo haiko katika mkataba wa leseni ya usafirishaji ni kitendo cha kuwaonea
Madereva na Wamiliki wa magari kwani kwa ratiba hiyo hulazimika kutembea
kilometa nne zaidi tofauti na njia ya awali.
Pia
Mwansasu amelisema kuwa njia hizo haziwasadii hata abiria wenyewe kwani kwa
safari ya kwenda mjini abiria wa Block T hupita Kabwe na anaporudi huachwa
Soweto hivyo kutonufaika na ratiba hiyo na kulazimika kutembea kwa miguu au
kutafuta usafiri mbadala.
Baada
ya majadiliano ya muda mrefu Madereva hao walikubaliana na Kamanda Msangi kwa
kurejesha huduma wakati suala hilo likisubiri majibu ndani ya siku mbili kutoka
Halmashauri ya Jiji na Sumatra ambao watakutana na Polisi wao kusimamia
taratibu zitakazopangwa.
Madereva
hao wlichukua fursa ya kumpongeza Kamanda wa Polisi kwa kudhibiti vitendo vya
rushwa barabarani ambavyo vilikuwa kero sugu na kuwafanya madereva kulichukia
Jeshi la Polisi kutokana na utendaji mbovu wa baadhi ya Askari wa Jeshi hilo
|
No comments:
Post a Comment