ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 18, 2014

KENYA YAONGOZA KWA WAFANYAKAZI WANAOINGIA NCHINI KINYEMERA NA KUFANYA KAZI KATIKA ZA KITAALUMA

KENYA YAONGOZA KWA WAFANYAKAZI WANAOINGIA NCHINI KINYEMERA NA KUFANYA KAZI KATIKA ZA KITAALUMA
Nchi ya Kenya imetajwa kuongoza katika orodha ya raia kutoka mataifa ya nje, wanaofikia thelathini na watano ambao wamekamatwa mkoani Arusha kwa kosa la kuishi nchini na kufanya kazi bila kibali, ikiwa ni takwimu za kuazia mwezi january hadi juni mwaka huu
Kenya inaongoza orodha hiyo kwa kuwa na raia wake kumi na watano huku raia watano wa Tanzania nao wakikamatwa kwa tuhuma za kuendesha mipango ya kushirikiana na wageni wa kutoka mataifa ya nje wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria
Wakati mashwali yakiwa mengi kuhusu njia zinazotumiwa na raia hao na wale wanaowafadhili,baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wanaona ikiwa vyombo vya usalama wa nchi havitakuwa macho huwenda tatizo hilo likawa kubwa zaidi
Suala la raia wa nje kuishi nchini bila
kibali pamoja na lile la wahamiaji haramu pia linatizamwa na wakazi wa mji huu kwamba huwenda likachochea kuibuka zaidi kwa vitendo vya kigaidi ambavyo vimeshuhudiwa katika siku kadhaa zilizopita
Mwaka jana matukio ya milipuko ya ma bomu wakati wa ibada ya ufunguzi wa kanisa la mtakatifu Joseph mfanyakazi Olasiti Arusha,mlipuko wakati wa kampeni za chama cha demokrasia na maendeleo chadema Soweto na mwaka huu mlipuko mwingine katika Baa ya Arusha night park ambapo kote huko vifo vya watu na wengine kadhaa kujeruhiwa viliripotiwa,wakazi wa mji huu wametaka wamevitaka vyombo vya usalama kuimarisha intelijensia yake zaidi
Jeshi la polisi likiwa ni chombo chenye jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao,kwa nyakati tofauti kimeelezea kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali zikiwemo za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa kadhaa wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi na ulipuaji mabomu lakini hawa bado wameonekana wote kuwa raia wa hapa hapa nchini
Idara ya uhamiaji nayo imesema hatua ambzao imekuwa ikizichukuwa ni kuwarudisha nchini kwao mara moja wale wanaobainika kuishi nchini kinyume cha taratibu na ikibidi kuwafungulia mashta pia wale wanaoonekana kufadhili mipango hiyo
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani idara ya uhamiaji zinaeleza kuwa tangu agizo la rais Jakaya kikwete lililoyataka makundi ya ujambazi,ujangili wamiliki wa silaha kinyume cha sheria kujisalimisha na wahamiaji haramu kurudi nchini kwao kwa hiari,jumla ya wahamiaji haramu 6,653 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa na kuchukuliwa hatua .

No comments: