WANANCHI zaidi
ya 500 wa Kijiji cha Moivaro na Chekereni katika Kata ya Moshono,
wilayani Arumeru wamelazimika kuendesha oparesheni ya kuwasaka wanaume
wanaolawiti wanaume wenzao baada ya kugundulika sehemu kubwa ya wanaume
katika kijiji hicho wamelawitiwa.
Inadaiwa kuwa kikundi hicho cha watu
zaidi ya saba kimekuwa kikiwalawiti wanaume wenzao wa rika mbalimbali
katika Kijiji cha Chekereni na Moivaro na kuwasababishia maumivu makali
sehemu ya makalio.
Hatua hiyo ilifuatia hivi karibuni mwanaume mmoja mwenye miaka 42 (jina tunalo) kulawitiwa hadi kupoteza fahamu na kukutwa mtaroni akiwa hajitambui.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kijijini hapo juzi (pichani), mwenyekiti wa mkutano huo,
Johnfas Molleli au Medoli
Molleli alisema kuwa upo uwezekano
mkubwa kwa wanaume wengi katika kijiji hicho walishalawitiwa ila
wamekuwa waoga kujitokeza kutokana na aibu.
Molleli alisema kama kuna wanaume
waliokumbwa na kadhia hiyo kuweka uwoga pembeni na kujitokeza kwenda
kupima hospitalini ili kubaini iwapo hawajaambukizwa magonjwa ya zinaa.
“Hapa kwenye mkutano wapo wanaume wengi
ambao wamelawitiwa na hilo kundi ila mmekuwa waoga kujitokeza.
Ninachotaka kuwaomba kapimeni afya zenu ili mjitambue kama mmeambukizwa
magonjwa ya zinaa,’’ alisema mwenyekiti huyo.Katika oparesheni hiyo,
wananchi walifanikiwa kuwatia mbaroni vijana
wanne, Richard, Stephano, Furaha na
Paulo huku wengine wawili, Thobias na mwingine aliyefahamika kwa jina la
Baba wanaendelea kusakwa wakiwa wote ni wakazi wa vijiji hivyo.
Molleli alisema kuwa kabla ya oparesheni
hiyo watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi
Chekereni na kufunguliwa mashitaka ya kulawiti jalada namba
Teng/RB/570/2014, lakini siku moja baadaye waliachiwa huru, ndipo wana
kijiji hao walipojikusanya na kuanzisha oparesheni ya kuwasaka na
kufanikiwa kuwakamata hao.
Watuhumiwa hao walipohojiwa katika mkutano wa hadhara walikiri kujihusisha na matukio ya ulawiti wanaume wenzao.
Baada ya maelezo ya watuhumiwa hao, mwenyekiti huyo aliwakabidhi mikononi mwa jeshi la polisi Kituo Kikuu cha Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP
Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema suala
hilo bado lipo kwenye uchunguzi.
>>>GPL
No comments:
Post a Comment