Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ambaye ni mmoja wa
wanamuziki wakongwe Tanzania hajamshawishi Linex Sunday Mjeda ambaye
amehoji mchango wake kwenye muziki.
Linex ameandika mtazamo wake kupitia akaunti yake ya Facebook na
Twitter, siku moja baada ya Sugu kumtuhumu Zitto Kabwe kwa kile
alichokiita ufisadi katika TANAPA na
NSSF kupitia kampuni ya
Lekadutigite Ltd inayomilikiwa na wasanii wa Kigoma All Stars, akiwemo
Linex.
“Hivi toka Sugu amekua mbunge ni kitu gani alishawahi kuwafanyia
wasanii wa Taifa hili, Tanzania na akiwa kama waziri kivuli, amewahi
kufanya nini kuinua kipato cha wasanii? Je amejenga mazingira gani
kuhakikisha wasanii hawawi ombaomba wakutegemea misaada bali
wajasiriamali?
"Eg. Amefikia wapi kwenye suala la hakimiliki na ufuatiliaji wake etc nimeuliza tu manaake kuna vitu vinaendelea sivielewi
No comments:
Post a Comment