Baadhi ya watoto wa shule za
msingi jijini Dar wakifanya mazoezi ya maigizo kwa ajili ya tamasha la
kesho kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Na Mwandishi wetu
WANAFUNZI wa shule za Msingi nchini,
wameshauriwa kuwa na mazoea ya kusoma vitabu kwa lengo la kuwa
wagunduzi wa vitu mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Soma, Demere Kitunga wakati wa
maandalizi ya tamasha la kwanza la vitabu vya hadithi kwa watoto wa
Shule za msingi.
Kitunga amesema kuwa tamasha hilo ni
moja ya michakato ya kuwataka watoto kupenda kusoma vitabu hasa vitabu
vya hadithi kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii.
"Ugunduzi wa jambo fulani unaanzia
katika kusoma hivyo watoto wakiwa wanania ya kusoma vitabu mbalimbali
hususani vya hadithi wataweza kuongeza uwelewa fulani katika fikra
zao,"amesema Kitunga
Aidha amesema kuwa tamasha hilo
linatarajia kuanza kesho hadi juni 14 mwaka huu katika viwanja vya
Makumbusho ya Taifa jijini ,ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete.
Mmoja wa watoto akionyesha kipaji
chake wakati wa mazoezi kwa vitendo kupitia hadithi mbalimbali
walizosoma kutoka kwenye vitabu.
Kitunga amesema kuwa Taasisi hiyo
hadi sasa imeweza kusambaza vitabu katika Shule mbalimbali za Msingi
pamoja na klabu za kujisomea zikiwemo Kurasini ,maktaba pamoja na
Chang'ombe.
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa
na maigizo ambayo yatafanywa kwa kutumia hadithi zilizokuwa katika
vitabu hii yote kwa lengo la kukuza utamaduni wa watoto kusoma vitabu.
No comments:
Post a Comment