ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 11, 2014

Mamilioni waukimbia mji wa Mosul Iraq


Mamilioni wanakimbilia usalama wao katika maeneo salama
Takriban watu nusu milioni wanaripotiwa kuukimbia mji wa Mosul, Nchini Iraq, ambao sasa unadhibitiwa na wapiganaji wa madhehebu ya Sunni.
Wapiganaji wa kiislamu nchini humo wanaendelea na
makabiliano yao ya kulidhibiti taifa hilo, hatua ambayo Marekani inaelezea kuwa ni hatari kubwa katika eneo hilo.
ISIS, ni mojawepo ya kundi lililomeguka kutoka kwa mtandao wa Al Qaeda ambalo linadhibiti eneo kubwa la mashariki mwa Syria, magharibi na katikati mwa Iraq na sasa yametwaa kabisa miji ya Kirkuk Salaheddin Nchini Iraq.
Waziri mkuu Nuri al-Maliki, ameliomba bunge litangaze hali ya hatari.

No comments: