
Mtakuja Beach, Beatrice Mhina nae akisistiza jambo kwenye semina hiyo.

Stori: Na Richard Bukos
MWANAMITINDO maarufu ulimwenguni na mshindi wa taji la Miss Tanzania
mwaka 2001, Happiness Magese, kupitia mradi wake wa Millen Magese
Foundation, leo amewapa semina wasichana wa shule za sekondari Mtakukuja
na Kondo pamoja na wasichana wa shule za msingi Mtakuja na Mtongani juu
ya ugonjwa wa Endometriosis ambao huwatesa wanawake wengi kwa maumivi
makali na pengine ugumba.
Mwanamitindo huyo alitoa somo hilo kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi
Mtakuja ambapo watu zaidi ya 1200 walielimishwa juu ya ugonjwa huo na
kupewa mbinu za kujilinda.
Katika semina hiyo, Happiness alijumuika na wasichana hao ambapo mara
nyingi wasichana hao walipokuwa na sura za huzuni kuhofia ugonjwa huo
aliwachangamsha kwa kucheza nao muziki.
(PICHA RICHARD BUKOS / GPL)
No comments:
Post a Comment