Timu ya New York
Timu ya DMV
Na Mwandishi wetu, New York
Mechi ya Vunja jungu inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa kabumbu wa New York na vitongoji vyake imeaanza maneno ya chini chini hasa kutoka kwa wachezaji wa timu ya New York wanaosema kwamba kufungwa kwao DC timu ya DMV isichukulie mechi ile kama kipimo cha wao kuidharau timu ya New York. Mpira wetu ni wa kiwango cha juu na wachezaji wenye umri mdogo. DMV walibahatisha tu mechi ile lakini wakija huko hawachomoi.
Mpambano huu wa marudiano wachezaji wengi wa timu hizi mbili wapo kimya sana tofauti na mechi iliyopita ambako wachezaji walitambiana sana kwenye mitandao ya kijamii na
hii labda ni baada ya matokeo ya mechi iliyopita ambayo timu ya DMV ilijipatia ushindi mnono wa bao 5-0.
Timu ya New York imepania sana mechi hii ya marudiano itakaychezewa New York siku ya Jumamosi June 28, 2014 kwa sasa timu zote zipo kwenye mazoezi japo sio kama wakati wa mechi yao ya kwanza ambako timu zote zilikuwa zikiweka picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na kutokana na mechi ya kombe la Dunia limepunguza kwa kiasi fulami kasi ya timu hizi kufanya mazoezi.
Timu ya DMV itaondoka kuelekea New York siku ya Jumamosi June 28, 2014 Alfajiri na mapema timu itaondokea 6200 Ager Road, Hyattsville, Maryland saa 12 asubuhi na wachezaji wapo kwenye hali nzuri ya mchezo na wamepania kulinda heshima ya mabao 5-0 waliyopata kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa DC siku ya May 24, 2014 katika uwanja wa Walker Mills Park.
Timu ya New York wamesema wao ndio mabingwa wakanda hii ya pwani ya mashariki kufungwa na DMV waliteleza tu na kuwaonya DMV wasubili kichapo siku hiyo na kuwapa mashabiki wa New York Vunja Jungu maridhawa.
Mpaka sasa hizi timu ya New York haijataja uwanja mechi hii itakapochezwa lakini habari za ndani zinasema mechi hii huenda ikachezewa kwenye uwanja wao unaojulikana kama machinjioni uwanja uliochezewa mechi yao na Boston na timu ya New York kuibuka na ushindi wa bao 7-1. Timu ya DMV wao wamesema hawaigopi timu ya New York hata wakituamsha usingizini bado watakula kichapo wachezaji wetu ni wazoefu na mechi hizi timu ya New York bado haijazoea mikikimikiki, bado changa ilibahatisha tu kuwafunga Boston.
Wataalam wa soka na ambao wanazifahamu timu za Kitanzania wameonya timu ya DMV kwamba wasibweteke na ushindi mnono walioupata DC kawaida unapokwenda ugenini huendi na wachezaji wote kwa hiyo inatakiwa iwe makini na ihakikishe inasafiri na wachezaji wote wazuri bila hivyo ngoma inaweza ikawageukia kwa sababu timu ya New York itakuwa nyumbani na wachezaji wake wote wakiwemo wale walioshindwa kusafiri na timu kuja DC.
Wachezaji wa DMV wapo katika hali nzuri na mchezaji Libe ameishaanza mazoezi mdogo mdogo na yupo tayari kucheza mechi hiyo na kiuongo wa DMV aliyeng'ara kwenye mechi ya kwanza Emma ameahidi kuonyesha kiwango cha kombe la Dunia kwenye mechi hiyo ya marudiano kati ya New York na DMV itakayochezwa June 28, 2014.
Makocha wa timu zote wapo kimya mpaka sasa hizi labda ni kwasababu wanajaribu kupanga mikakati mipya ya jinsi gani watakavyoingiza timu zao kwenye mechi hiyo ili waibuke na ushindi.
3 comments:
hawana lolote hao wakate rufaa wasikate hawana chao kwa dmv wakale halua na tende.
wache kusema sema kama ma binti ndo watakuja kukata rufaa washinde
SHIKENI ADABU ZENU WOTE MLEO WEKA COMMENT ZENU ZA KIBAGUZI NA KIJINGA JINGA CHUKI BINAFSI ZIMEKUSHIKENI NDANI YA NAFSI ZENU.KUSHINDA NA KUSHINDA NI MATOKEO NA SI ETI LEO MTU AKISHINDWA MUNAMSAKAMA NA KUMKEJELI. KWALIPI NA KAMA MNASOKA KWELI MBONA HAMUENDI WORLD CUP.MSHOHAYA WALA MSOONA VIBAYA.
Post a Comment