RAGE NAYE AUNGANA NA WANACHAMA SIMBA, DOKTA NDUMBARO, UCHAGUZI PALEPALE JUNI 29
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage ametumia busara kuu kwa kumuomba Rais wa
TFF, Jamal Malinzi, uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.
Rage amethibitisha kuandika barua hiyo huku akisema uchaguzi ukifanyika Juni 29 itakuwa ahueni kwa Simba.
Rage ambaye ni Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza leo mjini Dodoma na kusema tayari amewasilisha barua hiyo kwa Malinzi.
“Najua Malinzi ana madaraka katika hilo, ila vizuri Simba ifanye uchaguzi Juni 29 ili iweze kumaliza mambo yake mengine.
“Nimemuomba Malinzi, naomba mnielewe jamani nimemuomba ili asitishe uamuzi wake wa kusogeza uchaguzi mbele” alisema.
Juzi,
Malinzi alisema amesitisha uchaguzi huo hadi hapo itakapoundwa kamati
ya rufaa ndani ya Simba, kitu ambacho siku iliyofuata kilipingwa na
kamati ya uchaguzi, iliyosisitiza uchaguzi uko palepale Juni 29.
Lakini jana usiku kukawa na taarifa Rage anataka kuvunja kamati ya uchaguzi.
Alipozungumza leo akasisitiza: “Kamati ya utendaji imemaliza muda wake, hivyo haiwezi kufanya kazi ya kuteua kamati ya maadili.”
Wanachama
wa Simba, walimuonya Rage leo asubuhi asiungane na Malinzi na kubadili
tarehe ya uchaguzi, kitu ambacho anaonekana kutumia busara na
kuwasilikiliza.
chanzo: Saleh Ally
No comments:
Post a Comment