Bw.Mussa Leonard Mdede Aliyesimama.
Rais wa chuo kikuu cha CUHAS (Bugando) na
Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu nchini (TAHLISO), Bw.Mussa Leonard Mdede ameokotwa usiku huu katika maeneo ya Usagara nje kidogo ya jiji la Mwanza, akiwa amepoteza fahamu (hajitambui) lakini hana majeraha yoyote na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya vipimo na kupatiwa matibabu.Kwa sasa ameweza kuongea (japo kwa taabu) lakini hakumbuki chochote kilichotokea.

Bw.Mdede alitoweka ghafla siku ya jumatano tar.18 mwezi huu,
saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja yupo wapi, mpaka usiku huu
taarifa za kupatikana kwake zilipotolewa.Taarifa hizi zimedhibitishwa na Waziri
Mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Bw.Benjamin Thomas. Taarifa zaidi
juu ya hali ya Bw.Mdede zitazidi kutolewa kwa kadri zinavyopatikana.
Mkuu wa Upelelezi
Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.
SOURCE: Nicholaus Kilunga (mwandishi aliyepo mkoani Mwanza)

No comments:
Post a Comment