ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 11, 2014

Tahadhari kuhusu matapeli wanaotumia jina la JKT

TANGAZO

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma kuepukana na matapeli wanaochukua fedha kwa lengo la kuwapatia vijana nafasi za kujiunga na JKT. Nafasi za kujiunga na JKT haziuzwi popote.

Jeshi linaomba umma utambue kuwa linaendehsa mafunzo aina mbili. Aina ya kwanza ni Kujitolea na aina ya pili ni Mujibu wa Sheria.

Nafasi za vijana wa kujitolea zinatolewa na Mkuu wa JKT kupitia Wakuu wa Mikoa Tanzania Bara na
Visiwani. Aidha, Wakuu wa Mikoa huzigawa nafasi kwa Wakuu wa Wilaya, nao Wakuu wa Wilaya hugawa katika Tarafa, Kata na Vijiji vyao.

Aina ya pili ni Mujibu wa Sheria kwa vinaja wanaohitimu Kidato cha Sita katika mwaka husika na majina yao yanatolewa na Wizara ya Elimu na Utamaduni kupitia Baraza la Mitihani Tanzania.

Jamii inatahadharishwa kuacha kutoa fedha kwa matepeli kwa nia ya kupata nafasi za kujiunga na JKT. Kutoa au kupokea Rushwa ni kinyume cha sheria. Hivyo mtoaji na mpokeaji wakigundulika watashughulikiwa kisheria.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JKT

No comments: