
Serikali imewataka askari wa USalama BArabarani, maarufu kama Trafiki,
kuacha mara moja tabia ya kujificha vichakani na kujitokeza ghafla
kusimamisha magari yanayokwenda mwendo kasi.
Kauli hiyo ilitolewa
Bungeni jana na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima aalipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Musoma Mjini
Vincent Nyerere (CHADEMA).
Katika
maelezo yake Silima alisema “kama lengo la askari ni kukaa katika
vichaka kwa ajili ya kujikinga na jua kali hiyo ni sawa, ila si
kusimamisha magari kwa mtindo huo. Sheria zipo wazi iwapo itathibitika
kuwa askari wa usalama barabarani amesababisha ajali.”
2 comments:
Sioni tatizo trafic kujificha. Huo ni kawaida. Hata wenzetu US traffic wao anajificha kuna sa wahalifu.
nafikiri huu ni mtindo au mbinu wanazotumia maaskari kuwastukizia wavunja sharia. hata Marekani ni hivyo hivyo wanajificha msituni na camera zao hata magari yao ni ya rangi ya msitu. Madereva wafuate sharia na ndio solution.
Post a Comment