Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewaomba wabunge wa Bunge hilo kuweka maslahi ya Taifa mbele ili kutokomeza tabia chafu za viongozi wa serikali wanaotumia vibaya madaraka na kuliingiza Taifa katika hasara.
Kauli hiyo ilitolewa Msemaji Mkuu wa kambi hiyo katika Wizara ya Fedha na Uchumi, James Mbatia, wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 Bungeni jana.
Mbatia alisema katika kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi, wabunge wanao wajibu wa pamoja wa kuweka maslahi ya taifa mbele, na siyo itikadi za vyama, ili kuwatendea wananchi wote haki ya kukuza na kustawisha utu wao binafsi na utu wa Taifa.
”Ni rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuomba Bunge hili tukufu kutokomeza tabia, hulka na matendo yote yanayoashiria ubabe wa baadhi ya viongozi wa serikali, wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa na kuliingiza Taifa katika hasara,” alisema Mbatia.
Mbatia aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuhakikisha inaweka mifumo inayofaa na ya haraka katika kubaini na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, malipo yasioendana na makadirio, upotevu wa fedha zitokanazo maduhuli na ufanisi katika kuandaa na kutekeleza sera za mapato na matumizi ya fedha za serikali.
Alisema ripoti ya 2012/13 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imebainisha kuwa serikali ililipa Sh. bilioni 87.6 zaidi ya ilivyokadiria kwa ajili ya mishahara.
Ripoti hiyo, alisema inaonyesha kuwa serikali ililipa Sh, bilioni 173.9 zaidi ya ilivyokadiria ikiwa ni riba ya mikopo huku akitaka serikali kutoa majibu sahihi kuhusu sababu za kufanya malipo yasiyo katika makadirio ya serikali ya takribani Sh. bilioni 261.5 kwa mwaka huo wa fedha.
Mbatia pia alibainisha kuwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maduhuli kwa mwaka wa fedha 2012/13, serikali ilishindwa kukusanya mapato ya Sh. bilioni 190 kwa sababu za kimfumo.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilieleza kuwa deni la Taifa limeendelea kukua kila mwaka kutokana na Taifa kukopa kwa kasi kubwa kiasi ambacho dhamana za serikali zinaendelea kuwekwa rehani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment