Mmoja
wa walimu katika shule ya sekondari karema akipokea msaada wa vifaa vya
umeme kutoka kwa mbunge wa jimbo la mpanda Vijijini Moshi Kakoso ili
visaidie katika kuwapatia mwanga na kuongeza wigo wa kujisomea wakati wa
usiku na huduma nyingine za kijamii shuleni hapo.
……………………………………………………………………
Na Kibada Kibada –Katavi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Karema Wilayani Mpanda Mwambao
wa ziwa Tanganyika Mkoa wa Katavi wanakabiliwa na changamoto ya
usafiri shuleni hapo hali inayowafanya wakiugua ghafla usiku kupelekwa
hospitali kwa kulaza godoro juu ya toloRi na kupelekwa
Hospitali ili kupatiwa matibabu.
Hayo yamebainishwa na walimu katika shule hiyo wakati wakiwasilisha chanagamoto zao na kilio chao kwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso aliyefanya ziara ya kutembelea shule hiyo ili kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kupokea baadhi ya changamoto zinazo wakabili na kuzipatia ufumbuzi .
Awali Mkuu wa shule Osward Kalula
alitoa taarifa ya shule kuhusu maendeleo yaliyopo na changamoto
zinazowakabiri katika eneo lao kwenye taasisi hiyo na kueleza kuwa
baadhi yake ni ukosefu wa umeme, maji, vitabu, na usafiri, ambapo
changamoto ya umeme iliyopatiwa ufumbuzi hapo hapo na mbunge kwa
kukabidhi nyaya za umeme zenye mita miambili ili kusambazwa umeme katika
nyumba za walimu na mabweni, na madarasani kwa kutumia jenerata ndogo
ya shule iliyopo shuleni hapo.
Mbali ya kutoa nyaya hizo na vifaa
vingine vinavyohusiana na umeme ili vifungwe na umeme uanze kufanya
kazi na kuondoa kero ya ukosefu wa umeme pia Mkuu wa shule alipata
nafasi ya kushukuru kwa msaada huo ulotolewa na mbunge kwa kuonesha
jinsi anavyowajali wananchi wake na kujali elimukatika jimbo lake,pia
akawapa nafasi walimu kutoa changamoto nyingine zilizopo katika shule
hiyo kwa mwakilishi wao mbunge Kakoso.
Mmoja wa walimu katika shule hiyo Donatha Chamoto alieleza kuwa kwa kutolea mifano kuwa mwanafunzi mmoja aliugua usiku ikalazimika kubwebwa kwenye tololi kupelekwa hospitali usiku hali ambayo ni hatari kwa kuwa eneo shule ilipo na kituo cha Afya kilipo ni mbali kidogo.
Kutokana na tatizo hilo wanaomba kupatiwa usafiri japo hata bajaji itakayosaidia hata kuwa wanawapeleka hospitali pindi linapotokea tatizo la kuugua ghafla usiku kwa kuwa huwezi kujua lolote lawaza kutokea na hali ya hapo jinsi ilivyo ni tatizo kubwa walieleza.
Naye Diwani Kata ya Karema Maiko Kapata akashauri kuwa iwapo
usafiri wa gari ukikosekana wanaomba wapatiwe japo pikipiki za miguu
mitatu ili iwe inasaidia iwapo litajitokeza tatizo kama hilo kuliko
kuacha kama ilivyo sasa.
Akaongeza kuwa kwa kuwa sasa shule imepewa hadi ya kuwa na kidato cha tano na sita ni vyema serikali iakaangaliza namna gani ya kusaidia hata usafiri wa gari ili shughuli za kiutendaji ziweze kwenda vizuri kwani kutakuwa namajukumu ya kufuatilia makao makuu ya wilaya na pengine mkoani na upo umbali mkubwa zaidi ya kilometa 100 hadi kufika mpanda kutokea Karema ni mbali bila kuwa na usafiri wa uhakika inakuwa tatizo kwa kusubiria magari ya kudadia ni vyema Shule ikawa na usafiri wake wenye uhakika kulingana na majukumu yatakayokuwa yapo shuleni hapo.
Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso alishauri waangalie namna ya kuweza kupatiwa usafiri kwa kutumia mfuko wa jimbo wakae katika vikao waone namna ya kutumia fedha hizo
No comments:
Post a Comment