Endapo
umati uliofurika kwa wingi jana kumzika msanii mkongwe wa vichekesho
nchini marehemu Saidi Ngamba maarufu kama Mzee Small, ungechanga fedha
kwa ajili ya matibabu yake enzi za uhai wake, huwenda leo asingekuwa
marehemu.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wasanii wa bongo movie waliozungumza na eddy blog katika mazishi ya msanii huyo.
Jangala:
Kimsingi tumepata pigo kubwa sana kuondokewa na Mzee wetu, alikuwa
mbunifu na mwenye kuipenda kazi yake, hakuwahi kuifanya chini ya
kiwango, lakini leo hii maradhi yamemuondoa hatuna la kufanya zaidi ya
kumuomba Mungu ampokee na kumsamehe madhambi yake.
JB:
Wakati waze kama hawa wakiwa hai huwa hatuwatumii vipaji vyao vinapotea
bure, kiukweli kizazi cha sasa tunapaswa kuwatumia wazee hawa kabla
hawajafa, kuna wazee waliobaki kina King majuto, Bi Hindu na wengine
tusiwadharau
Steve
Nyerere: Laiti huu umati uliofika kumzika Mzee Small ungechanga hela
kwa ajili ya matibabu ya marehemu huwenda asingekufa kwa maradhi, ingawa
hatujui kama Mungu angempenda zaidi lakini ingetokea hivyo ni sawa pia,
lakini ni bora kumthamini mtu akiwa hai kuliko akifa kuuthamini msiba
wake, kwa kweli mimi nitawahsuri wenzangu tuwasaidie wakiwa wanaumwa
kuliko msibani.
Senga:
Nimefanya kazi na marehemu katika majukwaa kwa kweli uwezo wake ulikuwa
mkubwa hakuna haja ya kuukwepesha ukweli huu, tumepata pigo kubwa sana.
Richie:
Ni misiba ya mfululizo imetukumba wasanii, Mzee Small ni msanii mkubwa
sana, alikuwa na uwezo kwenye fani toka enzi hizo sisi ni wadogo
tunamuona akifanya vizuri hadi anakufa.
Mkwere:
Pengo la msanii yeyote ni ngumu kuzibika akishakufa hawezi kutokea kama
yeye, ikiwezekana kama watoto wa marehemu wanaipenda sanaa waingie ili
kuendeleza kipaji cha baba yao.
Mzee
Hashim kambi: Kiukweli Mzee Small alikuwa na uwezo katika sanaa ya
maigizo hasa vichekesho, kwa sasa hatunaye tena lakini tutamkumbuka
daima
Mzee Small aliugua kwa muda mrefu na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili
No comments:
Post a Comment