ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 5, 2014

WB : Uchafu waigharimu Tanzania Sh301bn

Dodoma. Utafiti uliofanywa nchini na Benki ya Dunia (WB), unaonyesha kwamba Serikali inapoteza Sh301 bilioni kwa mwaka kwa sababu na mazingira duni ya usafi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia moja ya pato la Taifa kwa mwaka.

Hayo yalisemwa jana na Meneja Mipango na Uendeshaji wa Programu ya Usafi wa Mazingira Tanzania (Umata), Mhandisi Koronel Kema. Programu hiyo inaendeshwa na Shirika la Kimataifa la Plan International. Alisema kama usafi wa mazingira utaboreshwa, fedha hizo zinaweza kuokolewa.

“Hizi fedha zingeweza kuokolewa na kutumika kufanya kazi nyingine kwa manufaa ya Taifa,”alisema.

Programu ya Umata inalenga kuboresha usafi wa mazingira kwa kuwezesha wananchi kujenga vyoo bora na kuvitumia.

Pia alisema mradi huo unalenga kuwawezesha watu kujenga tabia ya kunawa mikono kwa kutumia sabuni baada ya kutoka chooni. Kiwango hiki cha fedha, pamoja na sababu zingine kinatokana na tiba ambazo watu wamekuwa wakilazimika kugharimia kwa sababu ya kuathiriwa na magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Mwananchi

No comments: