Bw. Jin Guozhong, amemhakikishia Mheshimiwa Balozi Mdogo kuwa, nia yao ni kujenga uwanja wa maonyesho hayo ili kuwa kama kituo kitakachohudumia nchi zote za jrani na Tanzania. Waliomba kupata taarifa za mazingira ya uwekezaji Tanznaia, na tumekubaliana kuwa watafanya ziara nchini Tanzania katikati ya mwezi Agosti ili kukutana na Waziri wa Viwanda na Biashara na wadau wengine wote.
Mheshimiwa Balozi Mdogo Omar Mjenga akifanya mazungumuzo Chinese Chamber of Commerce of Dragon Mart, Dubai ambao wamekubali kuwekeza nchini Tanzania.
Bw. Jin Guozhong, Mwenyekiti wa Chinese Chamber of Commerce of Dragon Mart, Dubai.akimsikiliza Mheshimiwa Balozi Mdogo, Omar Mjenga wakati walipokua wakifanya mazungumuzo na wao kukubali kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Kikao kikiendelea
Mheshimiwa Balozi Mdogo akiwa na wageni wake. Anayesalimiana naye ni Bw. Jin Guozhong, Mwenyekiti wa Chinese Chamber of Commerce of Dragon Mart, Dubai. Wengine ni washauri wake wa masuala ya uwekezaji.




No comments:
Post a Comment