Advertisements

Friday, July 18, 2014

BAN KI MOON AMTEUA MJUMBE WAKE MPYA WA MAZIWA MAKUU

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon akiwa  Bw. Said Djinnit wa Algeria ambaye amemtangaza kuwa  Mjumbe wake Maalum   atakayeshughulikia Eneo la Maziwa Makuu. Bw. Djinnit anachuka  nafasi ya  Bi. Mary Robinson wa Ireland ambaye hivi karibuni   Katibu Mkuu amemteua kuwa mjumbe wake katika masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  akiwa  katika picha ya pamoja wa Wawakilishi wake ambao amewateua kushughulikia mgogoro wa Syria kushoto kwa  Katibu Mkuu ni  Bw.   Staffan de Mistura   na kulia kwa Katibu Mkuu ni  Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy  ambaye  ni  Makamu wa Bw. Mistura. Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi iliyoachwa na Bw.  Lakhder Brahimi aliyejiuzuru mwezi  Mei


Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua  Bw. Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake  maalum  atakaye shughulikia  Eneo la Maziwa Makuu. Bwana Djinnit anachukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye mapema wiki  alimtangaza kumteua kuwa  Mjumbe wake Maalum   kuhusu mabadiliko ya  tabia nchi ( Climate Change) 
Akitangaza uteuzi huo Ban Ki Moon, amemuelezea Bw, Djinnit kama mtu mwenye uzoefu mkubwa  na ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya  Umoja wa Mataifa na katika Umoja wa Afrika. Na kwamba  kutokana na uzoefu wake anamtarajia kutoa mchango mkubwa katika  mchakato wa  utafutaji wa Amani ya  kudumu katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Msimamizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi.  Pia amehudumu kama Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu nchini Nigeria,akisaidia   juhudi za kupambana na Boko Haram.
Djinnit ana uzeofu mkubwa katika masuala ya diplomasia, akiwa amewahi kuhudumu kama Kamishna wa kwanza  wa Organi ya   Usalama na Amani  ya Umoja wa Afrika ( AU) na kabla ya kuzaliwa upya kwa AU, aliwahi    Katibu Mkuu  Msaidizi wa  Masuala ya Siasa katika OAU ( Organization of African Union)
Wakati huo huo  Katibu Mkuu pia amewateua Bw.  Staffan de Mistura   kuwa  Mwakilishi wake Mpya  kuhusu  Syria  atasaidiana na pia amemteua Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy kama  makamu wake.    Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi ya Mwanadilomasia mzoefu na anayeheshimika Bw. Lakhder  Brahimi aliyejiuzuru  mwezi mei mwaka huu. Bw, Staffad de Mistura anakuwa  Mwakilishi wa tatu kuteuliwa kushughulikia mgogoro wa Syria, wa kwanza alikuwa ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Bw. Kofi Annan   ambaye naye alijiuzuru. 

1 comment:

Anonymous said...

Hivi UN hawaoni nini kinaenelea Middle east, inaonesha kama hawajali watu kufa, wanaendelea na yao kama kawaida..