
“Hawaogopi viongozi, anakwambia ‘niambie tatizo lako na nitalitafutia ufumbuzi kwa viongozi’. Hata ufundi pia ni mahiri sana, ninakuhakikishia tutakuwa tofauti sana msimu ujao.”
KOCHA mwenye msimamo kwenye maamuzi na asiyependa masihara katika nidhamu, Marcio Maximo, amemfanyia mabadiliko beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, anayekuwa kiungo sasa.
Lakini Twite amesema hajawahi kuona kocha mwenye tabia ya Maximo tangu aanze mpira na amekuwa akimshangaa katika kila kitu anachokifanya katika kikosi hicho.
Katika hayo anasema moja kubwa ni kwamba Maximo anapenda kuwa karibu na wachezaji wake na kuchukua matatizo yao.
Alisema Maximo amekuwa akijitahidi kutaka kujua matatizo ya wachezaji wake na kuyawasilisha moja kwa moja kwa uongozi jambo ambalo halikuwa likifanyika kwa makocha waliopita. Anasema matatizo wanayoyawasilisha, Maximo anahakikisha yanafanyiwa kazi kwa wakati.
“Yupo karibu sana na wachezaji hataki kuona mawazo yako yapo nje na kile anachotaka ukifanye, ni kocha bora sana kati ya niliowahi kukutana nao,” alisema Twite.
“Hawaogopi viongozi, anakwambia ‘niambie tatizo lako na nitalitafutia ufumbuzi kwa viongozi’. Hata ufundi pia ni mahiri sana, ninakuhakikishia tutakuwa tofauti sana msimu ujao.”
Katika mazoezi ya kikosi hicho juzi Jumanne na jana Jumatano katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola jijini Dar es Salaam ambayo ni maalum kwa ufundi wa uwanjani, Maximo alimpa Twite kazi ya kucheza nafasi ya kiungo mkabaji ikiwa ni dalili ya kutafuta tiba ya pengo la Frank Domayo aliyetimkia Azam FC.
Beki huyo ambaye amemtangaza Maximo kuwa ‘Bonge la Kocha’ alionekana kuendana na kasi anayoitaka bosi huyo kutokana na ubunifu ambapo muda wote Mbrazil huyo alionekana kumsifia kwa nguvu huku akisema: “Safiii...Twite safi saana.” Msaidizi wa Maximo, Leonardo Neiva, aliyepewa ruhusa ya kuzungumza badala ya mkuu huyo, alilianmbua Mwanaspoti kuwa kinachofanyika sasa ni kuangalia uwajibikaji wa kila mchezaji.
“Lazima tuwachunguze wachezaji wote, hilo tutaendelea nalo taratibu mpaka hawa wengine waliopo katika timu ya taifa watakapofika,” alisema.
Credit:Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment