Advertisements

Thursday, July 3, 2014

HARVARD CLUB OF WASHINGTON WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Harvard Club Of Washington, Bi. Caren A. Pauley akiutambulisha umoja wa wanafunzi waliowahi soma Chuo Kikuu cha Harvard waishio Washinton Metro Area kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula siku ya Jumatano July 2, 2014 umoja huo ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kukutana na jumuiya mbalimbali za Kitanzania na Taasisi zinazoshughulika na maswala ya Tanzania na kuweza kuongea pamoja kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Afisa Immaculata Diyamett anayeshughulika na maswala ya Utalii Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, akiwakaribisha wageni wote kwenye Tanzania House na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Rais wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Club Of Washington, Bi Yi-Fun Hsueh ambaye pia ni mmoja ya waratibu akiongea machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali kuwakaribisha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja kukutana na Jumuiya za Kitanzania na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujuana na kubadilishana mawazo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekanai Mhe. Liberata Mulamula akiwakaribisha Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Cha Harvard waishio Washinton Metro Area kikundi kinachobeba jina la  Harvard Club of Washington kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuwaelezea kuhusu Tanzania na vivutio vyake chini ni maelezo aliyokuwa akitoa Mhe. Balozi MSIKILIZE
Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi toka kwa Rais wa Umoja huo Bi. Yi- Fun Hsueh.
Rais wa Umoja huo Bi. Yi- Fun Hsueh akipokea zawadi toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Juu na chini Harvard Club Of Washington na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Balozi Libarata Mulamula.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Juu na chini Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na wageni waalikwa na kupata nao picha ya pamoja.
Juu na chini ni Mkuu wa Utawala na Fedha Mama Lily Munanka akiongea na wageni waalikwa na kupiga nao picha ya pamoja.
Juu na chini wageni waalikwa wakibadilishana mawili matatu wengine wakipata picha ya pamoja.

Balozi Liberata Mulamula akiwatambulisha wanafunzi Watanzania wa chuo hicho Belinda, Lawrence na Chikulupi
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly.
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mjumbe wa Jumuiya, mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, mwalimu wa Darasa la Kiswahili na mmoja wa Tano Ladies kwa wageni waalikwa.
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Greyson Kiondo
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Haika wa Mbezi Garden Hotel

Balozi Liberata Mulamula Justa wa Tano Ladies
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka.
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Bi.Karen B. Hoffman
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Afisa maswala ya Utalii Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Immaculata Diyamett
Balozi Liberata Mulamula Philip ambaye anaenda Tanzania kujiunga na kikundi cha TOA NAFASI PROJECT kinachosaidia watoto wa Tanzania chenye lengo na kuhakikisha mtoto wa Kitanzania anapata elimu japo ya msingi. Philip yeye amesema kazi yake ni kufundisha jinsi ya kucheza mpira na kuhakikisha watoto hao siku moja wataiwakilisha Tanzania kwenye kombe la Dunia mpira wa miguu.
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Carla ambaye naye atakuwa Tanzania siku za karibuni.
Balozi Liberata Mulamula akiwatambulisha Edward Taji na Bi Mariam Mkama ambao wapo kwenye kitengo cha VISA.
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Afisa Switibert Mkama
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Afisa Andrew Mgendi Zoka



No comments: