ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 3, 2014

KAMATI YA BUNGE YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA YAIWAGIA SIFA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KWA HUDUMA NZURI ZINAZOTOLEWA NA MFUKO HUO

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio (wa kwanza Kushoto) akiongea na wabunge wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakati wabunge hao walipotembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja Vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mh Luhoga J Mpina.
 Wabunge wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakisikiliza maelezo kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka Kwa afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele (mwenye suti nyekundu) wakati walipotembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam. Wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Mh William Erio (wa kwanza kushoto) akiwapatia maelezo ya ziada wabunge wa kamati ya Uchumi , Viwanda na Biashara wakati walipotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi , Viwanda na Biashara, Mh Luhago Mpina (aliyenyoosha mkono) akiuliza swali kwa Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati walipotembelea banda la PPF katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea kufanyika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akiwaonyesha Wabunge wa kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara michoro ya Majengo inayoonekana kwenye runinga (haipo pichani) yanayotarajiwa kujengwa na PPF ikiwa njia mojawapo ya uwekazaji utakaofanywa na Mfuko Wa Pensheni wa PPF.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh William Erio akiwaonyesha wabunge wa kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara miradi mbalimbali inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na mfuko huo wakati wabunge hao walipotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya Sabasaba aliyesimama ni Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

No comments: