Advertisements

Wednesday, July 30, 2014

MR.NICE AFUNGUKA SIRI YA KUFILISIKA KWAKE!

Stori: Shakoor Jongo
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ ameibuka na kufunguka kuwa siri ya kufilisika kwake ni kupenda kwake sifa kutoka kwa wapambe na matumizi mabaya ya fedha alizokuwa akiziingiza.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’.
Akizungumza na paparazi wetu, Nice, aliyetamba kwa staili ya Takeu, alisema wakati nyota yake ikiwa juu na kuingiza pesa nyingi kutokana na kupata shoo nyingi, alikuwa akitembea na kundi la mabaunsa, akibadilisha wanawake na kufanya matumizi makubwa yasiyo na lazima kwa lengo la kutaka sifa.
“Enzi zangu nani asiyejua kuwa nilikuwa natembea na kundi la mabaunsa, mademu na kila kumbi nikiingia basi kila mtu atajua kama Nice yuko ndani lakini mwisho wa sifa zile ni nini? Si ndiyo zimenifikisha hapa nilipo.

“Nilikuwa na kila aina ya kamati ya ufundi, mashehe, wachungaji na maaskofu, wote walikuwa wangu, lakini kwa kuwa nilikuwa nataka sifa, dua zao zilikuwa kazi bure kwa sababu nilikuwa mtu wa starehe,” alisema Mr. Nice.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasib Abdul,'Diamond Platinum' akila ujana.

NENO LAKE KWA DIAMOND
Katika kile kinachoonekana kama kumuonya staa wa sasa anayekimbiza katika Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’, alisema kwa kila ‘vurugu’ anayoifanya, yampasa kumtazama yeye kama mfano halisi endapo ataendekeza maisha ya anasa na kutaka sifa.

“Diamond kwa sasa anawika, anakubalika sana, ni kama ilivyokuwa kwangu. Namsihi asijisahau. Maisha yanabadilika. Namtakia mema ndiyo maana namshauri. Aachane na maisha ya kuwafurahisha watu, atengeneze maisha yake yajayo.

“Kuna wakati muziki unakataa, hapo ndipo mawekezo yake yatakapomfanya aendelee kuishi maisha bora bila muziki,” alisema Mr. Nice.
Credit:GPL

2 comments:

Anonymous said...

Ni kweli afadhali huyu ,kajisemea ,ukweli sababu ya wanawake.ni wanaume wachache ambao wanaona mbali .kitu cha kwanza wanafikiria nina hela .nitaakikisha napata msichana yule,kila siku anabadilisha wanawake kuja kushutuka .utakoma kuringa.

Anonymous said...

Acha kulalama, dust yourself up and move on kwani hiyo ndio hali halisi ya maisha.ups & downs are always there.