Advertisements

Tuesday, July 29, 2014

Palestina ipo tayari kusitisha mapigano-BBC

Uharibifu uliofanywa Gaza kutokana na vita
Uongozi wa Palestina umependekeza makubaliano ya saa ishirini na nne ya kusitisha mapigano dhidi yake na Israel.

Yasser Abed Rabbo wa chama cha PLO, Palestine Liberation Organisation amesema mpango huo umeungwa mkono na makundi muhimu likiwemo kundi la Hamas na la Islamic Jihad.

Hata hivyo mmoja wa maafisa wa Hamas Abu Zuhri amesema taarifa hiyo ya PLO haiwakilishi upande wa Hamas.

Mapema pendekezo la makubaliano ya kusitisha mapigano lililotangazwa, halikuweza kutekelezwa kwa kuwa hakuna upande wowote ulioweza kulitekeleza kwa kusitisha mapigano katika eneo la Gaza.

Bwana Rabbo amesema ujumbe wa pamoja unaoongozwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas utakwenda Cairo kuweka masharti ya kusitisha mapigano.

No comments: